Simu Yalipuka Na Kusababisha Moto Mkubwa Ndani Ya Bajaji

 





Njombe

Watu   wanne wamenusuriko kifo mara baada ya bajaji namba MC 567 CJK aina ya TVS iliyokuwa ikitoka maeneo ya stendi kuu ya mji wa Njombe kuelekea katikati ya mji kupinduka kutokana na mlipuko mkubwa wa simu ya abiria uliosababisha moto.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema bajaji hiyo imepinduka kutokana na dereva kugeuka nyuma kutokana na taharuki ya kulipuka kwa simu ndogo mali ya Siston Antony katika barabara kuu ya Njombe-Songea majira ya saa tano asubuhi.

“Moto umelipuka mkubwa na dereva wa bajaji akageuka kuangalia abiria wake na kushindwa kuiongoza akaiachia bajaji wakapinduka”amesema Kamanda Issah.

Kamanda Issah amesema baada ya ajali hiyo polisi imeweza kuingilia kati kutokana na mmiliki wa bajaji kutaka kulipwa na abiria mmiliki wa simu iliyosababisha mlipuko na kupelekea kupinduka kwa bajaji na kuharibika.

Aidha Kamanda Issa ametoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya moto kuwa na bima za vyombo vyao ili kuepusha usumbufu kama huo huku pia akitoa rai kwa wamiliki wa simu kuwa makini na matumizi ya simu zao,na kubainisha kuwa abiria wote waliweza kupelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu ya majeraha madogo na kuruhusiwa kutoka ili kuendelea na shughuli zao.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments