TAIFA STARS YAICHAPA 1-0 SOMALIA

 

TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Somalia, mchezo wa  hatua ya pili ya mchujo ya kuwania kufuzu Michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za ndani (CHAN) kwenye uwanja wa Banjamin Mkapa.

Mshambuliaji Mpya wa Azam FC  Abdul Suleiman ‘Sopu’ aliwanyanyua watanzania mnamo dakika ya 47 kipindi cha pili akifunga bao kwa Kichwa akipokea ‘Krosi’ safi ya Mlinzi wa pembeni, Kibwana Shomari..

Kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza, Timu ya taifa ya Somalia walikuwa nyumbani Benjamin Mkapa, Kikanuni kutokana na sababu za kiusalama nyumbani kwao. Mchezo wa mkondo wa pili utachezwa Julai 30, 2022 ambapo Taifa Stars itakuwa nyumbani kwenye uwanja huo huo wa Mkapa.

Taifa Stars inatakiwa kupata sare yoyote au ushindi ili kusonga mbele kwenye hatua inayofuata ili kujihakikishia nafasi nzuri ya kufuzu Michuano hiyo ya CHAN.

Mshindi wa jumla wa mchezo huo kati ya Taifa Stars dhidi ya Somalia atacheza na timu ya taifa ya Uganda (The Cranes) ambao utakuwa mchujo wa mwisho ‘Play Off’ ya kuwania kufuzu Michuano ya CHAN ambayo itafanyika nchini Algeria, kuanzia Januari hadi Februari, 2023.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments