TANGA UWASA YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA AJILI YA MASHINDANO YA UMITASHUMTA

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia akikabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya milioni 2 kwa Afisa Elimu Msingi Jiji la Tanga Kasim Kaonekana kwa ajili ya michezo ya Umitashumta iliyoanza leo kwenye shule ya Sekondari Tanga School

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly wa tatu kutoka kushoto na Afisa Elimu Msingi Jiji la Tanga Kasim Kaonekana wa tatu kutoka kushoto wakiwa jezi za traki suti vyenye thamani ya milioni 2 kwa kwa ajili ya michezo ya Umitashumta iliyoanza leo kwenye shule ya Sekondari Tanga School

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia akikabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya milioni 2 kwa Afisa Elimu Msingi Jiji la Tanga Kasim Kaonekana kwa ajili ya michezo ya Umitashumta iliyoanza leo kwenye shule ya Sekondari Tanga School

Na Oscar Assenga,TANGA.

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa) imetoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya Milioni 2 kwa ajili ya michezo ya Umitashumta kwa wanafunzi wa Jiji la Tanga inayoanza leo kwenye shule ya Sekondari Tanga School ili kuhakikisha michezo hiyo inafanyika kwa tija kubwa.

Halfa ya makabidhiano ya vifaa hivyo ilifanyika leo kwenye ofisi za Mamlaka hiyo ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly alimkabidhi Afisa Elimu Msingi wa Jiji hilo Kasimu Kaoneka kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la Tanga.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Hilly alisema wameamua kutoa msaada huo wa vifaa vya michezo ili kuweza kuunga mkono mashindano hayo.

Alisema wao Tanga Uwasa kama wadau wa elimu wanatambua umuhimu wa michezo katika elimu kwa ajili ya wanafunzi ili waweze kupata afya nzuri na kuweze kusoma vizuri kwa hiyo wamechangia katika kuhakikisha michezo hiyo inafanikiwa na wanafunzi wanafurahi.

Alisema wanatambua kuwa mazingira bora yanasaidia kuwa na elimu bora licha ya kuchangia michezo lakini wanachangia ujenzi wa madarasa na viti vingine ili kutenegenza mazingira mazuri ya elimu.

Awali akizungumza wakati akipokea vifaa hivyo Afisa Elimu Msingi wa Jiji la Tanga Kasimu Kaoneka ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Spora Liana alisema kwamba michezo ni kitu muhimu kwa wanafunzi kwani wanaenda shuleni kupata taaluma lakini sio taalima tu ni pamoja na michezo ambacho ni kivutio kimojawapo kina mfanya mwanafunzi aweze kwenda shuleni.

Alisema na hivyo kupitia michezo atapata na taaluma yake na hivyo anasisimua ubongo wake hatua inayopelekea kitu anachofundishwa anakipata kwa sababu mwili unakuwa upo imara na timamu kiakili.

“Tunawashukuru Tanga Uwasa kwa kutupatia vifaa hivi vya michezo na tunahaidia kwamba tutahakikisha tunaleta vikombe vingi na tutawakaribisha wakati wa kukabidhiwa”Alisema

Hata hivyo alisema michezo hiyo ngazi ya Kanda inaanza leo ambapo itahusisha wilaya za Mkinga,Pangani,Muheza na Tanga na yanafanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Tanga School

Naye kwa upande wake Kasimu Issa anayesoma Darasa la saba shule ya Msingi majani mapana alisema wanashukuru kwa msaada huo wa vifaa hivyo kuhakidi kwenda kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments