Ukataji Wa Tiketi Mtandao Wasuasua, Wapiga Debe Wahofia Vibarua

 Ikiwa leo ndio siku rasmi ambapo wadau wa usafiri wa masafa marefu walitakiwa kuanza rasmi mfumo wa ukataji wa tiketi kwa njia ya mtandao bado muitikio umekua wa kusuasua huku wapiga debe wakiendelea na kazi za ukataji tiketi za kawaida.

Mwananchi ilifika katika kituo kikuu cha Mabasi Moshi Mjini na kushuhudia wapiga debe wakiendelea na kazi yao ya kutafuta abiria na kuwakatia tikite za kawaida.

Mmoja wa wakataji wa tiketi katika stendi hiyo, Ally Abdallah amesema vijana wengi wanajihusisha na kazi ya kukatisha tiketi ambayo inawasaidia kupata rizki.

 "Madalali ndio wanahangaika kutafuta abiria na kuwezesha gari ijae ili iweze kuanza safari na kwa kazi hiyo tunaweza kusomesha na kutunza familia huu mfumo ukizingatiwa vijana wengi watakua vibaka maana udalali ndio kazi wanayoitegemea" amesema Abdallah

Amesema ni wasafirishaji wachache ambao wameweza kuupokea mfumo huo lakini wengi bado wanatumia mfumo wa zamani.

Ofisa Mfawidhi Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra) Mkoa wa Kilimanjaro, Paulo Nyello amesema kuwa kila kampuni inayojihusisha na usafirishaji itatakiwa kusajili watoa huduma wake ambao ni madereva na kondakta ambapo watatoa huduma ya kukata tiketi kwa kutumia mashine ya kimtandao ya kutolea tiketi.

"Tayari mamlaka imetoa maelekezo na sasa tunasubiri utekelezaji, tunafuatilia kujua kama zipo changamoto na kila kampuni itasajili watoa huduma wake ambao ni madereva na kondakta na hao ndio watakaotambulika." amesema Nyello

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments