Vodacoma Tanzania Foundation Yatuzwa Na Hospitali Ya CCBRT Kwa Mchango Wa Kujenga Wodi Ya Kina Mama Wajawazito Na Watoto

 -Ilichangia shillingi 8 bilioni kukamilisha wodi hiyo.


Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc kupitia asasi yake ya Vodacom Tanzania Foundation imepokea tuzo kutoka hospitali ya CCBRT ambapo wamekabidhiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu ikiwa ni shukrani kwa mchango wake wa kuwezesha kujenga wodi ya kina mama wajawazito na watoto wachanga kwa hospitalini hapo. kampuni hiyo iliwezesha ujenzi wa wodi kwa kutoa msaada wa shilingi 8 bilioni.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Rais Samia aliwapongeza Vodacom kwa kuwezesha suala hili na kwa namna gani wanajitoa kurudisha tabasamu kwa jamiii, huku akiongeza kwamba pamoja na hilo kampuni hiyo ina mradi wa m-mama ambao pia unalenga kuwasaidia wanawake wajawazito na watoto, hii inadhihirisha namna kampuni ya Vodacom iko karibu na jamii kupitia huduma za afya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Biashara Vodacom Tanzania Plc (aliyepokea tuzo hiyo kwa niaba ya asasi ya Vodacom Tanzania Foundation) Linda Riwa alisema “sisi kama kampuni ya mawasiliano tunajua wajibu wetu kwa jamiii na malengo yetu makubwa ni kurudisha kwa jamiii kwa kile tunachokipata, ndio maana kupitia sekta ya afya tumekuwa mstari wa mbele mno.”

Asasi ya Vodacom Tanzania Foundation inasaidia maeneo mbalimbali ya kusaidia jamii hususan kwenye afya ambapo inaweza kusaidia wagonjwa wa fistula na watoto njiti.



Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi tuzo kutoka hospitali ya CCBRT Mkurugenzi wa biashara wa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC Linda Riwa aliyepokea kwa niaba ya asasi ya Vodacom Tanzania Foundation ikiwa ni shukrani ya mchango wa shilingi 8 bilioni waliotoa wakati wa ujenzi wa wodi ya kina mama wajawazito na watoto wachanga hospitalini hapo, hafla ya ufunguzi wa jingo hilo ilifanyika  jijini Dar es Salaam.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments