WAFANYAKAZI WA HALMASHAURI NCHINI WAMETAKIWA KUFATA WANANCHI VIJIJINI ILI KUWASIKILIZA KERO ZAO BADALA YA KUWASUBILI MAOFISINI

Waziri mkuu  Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kufikisha huduma mbalimbali za jamii zikiwemo za afya kwa wananchi wote hadi waishio maeneo ya vijijini ili wazipate kwa wakati.

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo  Julai 16, 2022) wakati akizungumza na wananchi katika kata ya Mtoa wilayani Iramba baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha afya cha Mtoa akiwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani Singida.

Amesema kukamilika kwa kituo hicho kutawawezesha wananchi hao kupata huduma za afya zikiwemo za maabara, mama na mtoto na upasuaji karibu na makazi yao. “Mheshimiwa Rais Samia ameelekeza huduma za afya ziwafikie wananchi wote hadi waishio vijijini.”
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa nne kushoto) akivuta pazia kuashiria kuweka jiwe la msingi la mradi wa Kituo cha Afya cha Mtoa, kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mkoani Singida wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo leo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda, Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida Martha Gwau, Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk.Mwigulu Nchemba, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimbah, Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Festo Dugange na Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko.

Waziri mkuu  Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kufikisha huduma mbalimbali za jamii zikiwemo za afya kwa wananchi wote hadi waishio maeneo ya vijijini ili wazipate kwa wakati.


Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo  wakati akizungumza na wananchi katika kata ya Mtoa wilayani Iramba baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha afya cha Mtoa akiwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani Singida.

Amesema kukamilika kwa kituo hicho kutawawezesha wananchi hao kupata huduma za afya zikiwemo za maabara, mama na mtoto na upasuaji karibu na makazi yao. “Mheshimiwa Rais Samia ameelekeza huduma za afya ziwafikie wananchi wote hadi waishio vijijini.”

Waziri Mkuu amesema kwa wilaya ya Iramba, Serikali imeidhinisha shilingi bilioni 2.8 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya sita kwa lengo la kusogeza huduma hizo karibu na makazi ya wananchi.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameupongeza uongozi wa wilaya ya Iramba kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa kituo cha afya cha Mtoa, ambapo ameiagiza Wizara ya Fedha ya Mipango kupeleka kiasi cha shilingi milioni 262, 635,689 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo hicho
     
Kwa Upande Wake  Mwenyekiti Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Wa Singida Alhaji Juma Kilimba amewaomba wananchi wa Mkoa Wa Singida Kuendelea Kukiamini Chama Cha Mapinduzi Na Serikali Ya Awamu Ya Sita ,Kwani Imeendelea Kutekeleza Ilani Ya Chama Cha Mapinduzi Kwa Kuendelea Kuwafikia Wananchi Kwa Kuwaletea Huduma Mbali Mbali  Za Kijami Katika Maeneo Yao.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments