WIZARA YA NISHATI NA TAASISI ZAKE,YASHIRIKI MAONYESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA (SABA SABA) DAR-ES-SALAAM

Mdhamini wa Kampuni ya E-motion Afrika, Bw.Denis Leboutex (wa kwanza kulia), akizungumza na wataalam kutoka Wizara ya Nishati ili kuweza kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara wakati wa maonesho ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam, tarehe 03 Julai, 2022.

 Wataalam kutoka Wizara ya Nishati wakizungumza na mmoja wa mteja aliyefika katika Banda la Wizara wakati wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere.

 Meneja wa Kampuni ya E-motion Afrika Mha.Gilbert Minja inayoshughulika na ubadilishaji wa mifumo ya Magari yanayotumia Mafuta kwenda kwenye mfumo wa uendeshaji Magari yanayotumia Nishati ya Umeme iliyopo Jijini Arusha, akizungumza na wateja mbambali na kuwaelekeza namna mfumo huo unavyofanya kazi kwenye gari, wakati wa Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam, tarehe 03 Julai, 2022.
Meneja wa Mradi wa Gesi asilia Dkt. Esebi Nyari wa pili kushoto, kutoka taasisi ya teknolojia Dar es salaam (DIT), akizungumza na mmoja wa mteja aliyefika katika Banda la TPDC ili kupata maelezo ya kina kuhusu Mradi wa kufunga gari mfumo wa kutumia Nishati ya Gesi kwenye Magari, wakati wa Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam, tarehe 03 July 2022.

Wataalam kutoka Baraza la Ushauri la Watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA, yaani huduma za Maji na Nishati, wakizungumza na mmoja wa wateja waliofika katika Banda la mamlaka hiyo ili kuweza kufahamu shughuli zinazofanywa na mamlaka hiyo, wakati wa Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Jijini Dar es Salaam, Tarehe 03 Julai 2022

Watalaam kutoka Wakala wa Uagizaji wa Mafuta (Petroleum Bulk Procurement Agency), wakizungumza na mmoja kati ya wateja waliofika katika Banda la (PBPA) Bw.Fredick Kitosi ili kuweza kufahamu shughuli mbambali zinazotekelezwa

Mtalaam kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), akizungumza na mmoja wa wateja waliofika katika Banda la EWURA ili kufahamu shughuli mbambali zinazotekelezwa na mamlaka hiyo,wakati wa Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam Tarehe 03 Julai, 2022

Na Timotheo Mathayo 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments