Wawili wajiua Singida kwa sababu Za Kimapenzi

Wakazi wawili wa tarafa ya Sepuka, wilaya ya Ikungi mkoani Singida wamejiua kwa sababu tofauti za kimapenzi.

Watu hao ni kijana, Francis Juma (20) ambaye amekunywa sumu ya panya baada ya mchumba wake kumkataa pamoja na mzee mmoja, Hamisi Mdonko (70) mkazi wa kijiji cha Mtunduru ambaye amejinyonga hadi kufa baada ya kumnajisi mjukuu wake, mwanafunzi wa shule ya msingi.

Akizungumza na Mwananchi leo Julai 18, 2022, mama mzazi wa Francis, Esther Kitiku amesema mwanae amejiua mwishoni mwa wiki baada ya kunywa sumu ya panya aliyoichanganya na soda.

Amesema Francis alichukua uamuzi huo muda mfupi baada ya mchumba wake kukataa kuolewa naye wakati wakiwa kwenye kikao cha kukubaliana taratibu za harusi kilichofanyika nyumbani kwa binti huyo kijiji cha Mpugizi.

Ofisa mtendaji wa kijiji cha Masutianga tarafa ya Sepuka, Miraji Ntungu amekiri kutokea kwa tukio hilo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika tukio jingine, Mdonko (70) mkazi wa kijiji cha Mtunduru amejinyonga hadi kufa baada ya kumnajisi mjukuu wake ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika kijijini Mtunduru, wiki iliyopita wake zake wawili na Mzee Mdonko wakati wanatoka kuchota maji, walishituka baada ya kumkuta mume wao amening’inia kwenye mti huku akiwa amefariki.

Kaimu Ofisa mtendaji wa kata ya Mtunduru, Issa Yusufu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo. Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, ACP Stella Rutabihirwa, pia amekiri kutoka kwa matukio hayo mawili na wanaendelea na uchunguzi.

  Chanzo Mwananchi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments