Waziri wa Maji nchini Tanzania, Jumaa Aweso amemuagiza katibu mkuu wizara hiyo, Mhandisi Anthony Sanga kupunguza milolongo isiyokua ya lazima ili kuhakikisha utekelezaji wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda mkoani Simiyu unakamilika kwa wakati.
Mradi huo unaogharimu Sh400 bilioni.
Akiwa katika ziara ya kukagua mabonde ya maji mkoani Simiyu, leo Ijumaa Julai 29, 2022 amesema Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kujenga visima lakini kwa maeneo haya pesa hiyo inapotea hivyo njia pekee na suruhu ya changamoto ya maji katika mkoa wa Simiyu ni utumiaji wa maji katika ziwa Victoria lakini mradi umechukua muda mrefu sana.
"Tunatambua kabisa sasa tupo hatua ya kumpata mkandarasi lakini michakato ya kimanunuzi ambayo siyo ya lazima tuachane nayo ili kuweza kuwahisha huduma ya maji safi na salama kwa wananchi," amesema Aweso.
Aidha, amewaagiza wakurugenzi wa mabonde tisa ya maji nchini kuzishirikisha kikamilifu jamii katika utunzaji wa vyanzo vya maji ili kujua umuhimu wa vyanzo hivyo katika uendelevu wa miradi ya maji.
Mkurugenzi wa raslimali maji kutoka wizara ya maji, Dk George Lugomela amesema ili kutunza raslimali za maji mkoani Simiyu Serikali imewekeza katika kulinda na kuhifadhi chanzo cha maji cha new Sola wilayani Maswa ambapo kimechangia upatikanaji wa maji kwa asilimia 68 likihudumia mji wa Maswa na vijiji 11.
Waziri Aweso aagiza kuharakishwa miradi ya maji bonde la Ziwa Victoria
FRIDAY JULY 29 2022
Maswa. Waziri wa Maji nchini Tanzania, Jumaa Aweso amemuagiza katibu mkuu wizara hiyo, Mhandisi Anthony Sanga kupunguza milolongo isiyokua ya lazima ili kuhakikisha utekelezaji wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda mkoani Simiyu unakamilika kwa wakati.
Mradi huo unaogharimu Sh400 bilioni.
Akiwa katika ziara ya kukagua mabonde ya maji mkoani Simiyu, leo Ijumaa Julai 29, 2022 amesema Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kujenga visima lakini kwa maeneo haya pesa hiyo inapotea hivyo njia pekee na suruhu ya changamoto ya maji katika mkoa wa Simiyu ni utumiaji wa maji katika ziwa Victoria lakini mradi umechukua muda mrefu sana.
"Tunatambua kabisa sasa tupo hatua ya kumpata mkandarasi lakini michakato ya kimanunuzi ambayo siyo ya lazima tuachane nayo ili kuweza kuwahisha huduma ya maji safi na salama kwa wananchi," amesema Aweso.
Aidha, amewaagiza wakurugenzi wa mabonde tisa ya maji nchini kuzishirikisha kikamilifu jamii katika utunzaji wa vyanzo vya maji ili kujua umuhimu wa vyanzo hivyo katika uendelevu wa miradi ya maji.
Mkurugenzi wa raslimali maji kutoka wizara ya maji, Dk George Lugomela amesema ili kutunza raslimali za maji mkoani Simiyu Serikali imewekeza katika kulinda na kuhifadhi chanzo cha maji cha new Sola wilayani Maswa ambapo kimechangia upatikanaji wa maji kwa asilimia 68 likihudumia mji wa Maswa na vijiji 11.
Mikakati wa kulinda chanzo hicho ikiwa ni pamoja na kutengeneza mazingira ya wafugaji ambao ndio wakazi wengi wa jamii hiyo kuwa hawapeleki mifugo katika chanzo cha maji kwa kujenga mabirika ya kunyweshea mifugo katika vijiji vinavyozunguka eneo la bwawa.
"Mafanikio ya bwawa hili ni pamoja na kupunguza gharama za matumizi ya dawa za kutibu maji kutoka Sh 15 milioni hadi Sh 5 milioni hivyo pesa hiyo itatumika kuchangia gharama za umeme ili kuongeza upatikanaji wa maji," amesema Dk Lugomela
Akiwa katika uzinduzi wa mradi wa kutibu maji wilayani Maswa mkurugenzi wa Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira wilaya ya Maswa (Mauwasa) Nandi Mathias alisema mradi huo unauwezo wa kuzalisha maji meta za ujazo 10,380 kwa siku.
"Lengo ni kufikia uzalishaji maji kwa asilimia 90 ifikapo 2025 ili kukidhi mahitaji ya maji kwa wananchi," alisema
0 Comments