YANGA SC YAMTAMBULISHA BIGIRIMANA, ALIWAHI KUCHEZA NEWCASTLE UNITED

 Yanga Sc imemtambulisha Kiungo wa Kimataifa wa Burundi, Gaël Bigirimana ambaye amewahi kucheza Klabu ya Newcastle United ya nchini Uingereza, kati ya mwaka 2012-2016, pia amewahi kucheza Coventry City FC ya nchini humo.


Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akitambulishwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa timu hiyo, Bigirimana amesema kuwa amekuja nchini kucheza soka Young Africans SC, amesema muda umefika kucheza kwenye Klabu hiyo ya Wananchi.

“Sijaja kunyonya timu, nimekuja kutumikia timu, nimecheza soka Ulaya, na nimepata ofa nzuri lakini kutokana na mipango ya Rais wa Klabu (Hersi) naamini hapa ni mahala pa kutimiza kazi zangu”, amesema Bigirimana.

Pia, Bigirimana amewahi kucheza Rangers FC ya Scotland, mara ya mwisho kabla ya kutua Yanga SC alikuwa anacheza timu ya Glentoran FC ya Ireland.

Kwa upande wake, Rais wa Klabu hiyo, Mhandisi Hersi Said amesema wanaendelea kuijenga Yanga SC iliyo bora siku za mbeleni na kuhakikisha inafanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali ambayo timu hiyo inashiriki.

“Tunataka kutangaza Mchezaji mmoja Saa 9 Usiku, sisi hatupangiwi muda wa kutangaza Mchezaji tunayesajili, lakini kuna mmoja alicheza Royo Volcano, kuna mwingine anatoka Magharibi mwa Afrika”, amesema Rais wa Klabu.

Yanga SC imeahidi kusajiliwa Wachezaji watano wa Kimataifa wakiwemo Nyota wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephene Aziz Ki, na Beki wa Kushoto, raia wa DR Congo, Joyce Lomalisa Mutambala ambaye amecheza timu ya Grupo Desportivo Interclube ya Angola.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments