CCM YAMUAGIZA WAZIRI WA KILIMO KUMUONDOA MRAJISI VYAMA VYA USHIRIKA TABORA

Katibu wa nec ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akipiga Ngoma baada ya kuzungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mfuluma, Wilaya ya Uyui mkoani Tabora akiwa katika ziara ya kukagua Uhai wa chama na Utekelezaji wa Ilani ya I chaguzi ya CCM ya 2020-2025. (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).
Katibu wa nec ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mfuluma, Wilaya ya Uyui mkoani Tabora akiwa katika ziara ya kukagua Uhai wa chama na Utekelezaji wa Ilani ya I chaguzi ya CCM ya 2020-2025. (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).
Katibu wa nec ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akipata maelezo kuhusu karakana ya SIDO Mkoa wa Tabora kutoka kwa Meneja wa SIDO wa mkoa huo, Samuel Neligwa, akiwa katika ziara ya kukagua Uhai wa chama na Utekelezaji wa Ilani ya chaguzi ya CCM ya 2020-2025. (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).

Ni kutokana na kudaiwa kuwa chanzo cha kukwamisha usajili wa vyam vya msingi kwa wakulima wa tumbaku

Shaka apigilia msumari wa mwisho...CCM haitokubali kuona mkulima akiendelea kuteseka Na Mwandishi Wetu, Tabora,Agosti 19, 2022.

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka amemuagiza Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kumuondoa haraka Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tabora kwa madai amekuwa chanzo cha kukwamisha jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan za kuwainua wakulima wa zao la tumbaku na kusaabisha malalamiko kwa wakulima wa mkoa huo .

Shaka ametoa maagizo hayo leo Agosti 19,2022 wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ufumula wilayani Uyui mkoani Tabora ambapo akiwa hapo alipokea malalamiko mbalimbali ya wakulima wa zao tumbaku na miongoni mwa malalamiko ni ya kuwepo kwa urasimu wa kusajiliwa vyama vya msingi(AMCOS).

Akizungumza wakati anatoa maagizo hayo Shaka amesema amepokea malalamiko ya Mrajisi wa vyama vya ushirika mkoa wa Tabora Geophrey Chiliga kuwa na changamoto mbalimbali zinazokwamisha jitihada za wakulima.

“Changamoto za bwana huyu imekuwa donda sugu , tumetoka Kaliua analalamikiiwa, tumetoka Sikonge analalamikiwa, tumetoka Urambo analalamikiwa, leo tuko Uyui watu wanalia na huyu bwana. Urasimu umekuwa mkubwa sana.

Shaka amesisitiza Waziri wa Kilimo watamjulisha kwamba Mrajisi huyo hafai kuwa Tabora na hivyo wampangie majukumu mengine sehemu ambayo hakulimwi kilimo cha tumbaku aende akafanye anavyotaka lakini sio Tabora.

Tutalinda jasho lenu lakini tutalinda jitihada za Rais Samia anazoziweka ili kukuza zao hili la tumbaku,”alisema Shaka.

Amesema zao la tumbaku linawaheshimisha wana Tabora, limekuwa mkombozi kwao na Rais Samia ameongeza ushindani katika ununuzi kutoka kampuni mbili mpaka kampuni sita halafu, halafu anatoa mjanja mmoja anataka kukwmaisha jitihada hizo na CCM hakiwezi kukubali , hivyo watalala naye mbele.

USHAURI WA CCM KWA WIZARA YA KILIMO KUJENGA KIWANDA. CHA KUCHAKATA TUMBAKU, KUTENGENEZA SIGARA WAKATI HUO HUO

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshauri na kupendekeza kwa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kujenga kiwanda cha kuchakata tumbaku pamoja na ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza sigara ndani ya Mkoa wa Tabora kwani kuna kila sababu ya kuwa na viwanda hivyo kutokana na mkoa huo kuwa kinara wa zao hilo nchini.

Amefafanua Tabora imeongoza uzalishaji tumbaku kutoka kilo milioni 16 mpaka kilo milioni 33 rai ya CCM kwa Wizara ya Kilimo umefika wakati wa kuangalia haraka iwezekanavyo kujenga kiwanda cha kuchakata tumbaku mkoani Tabora kwani ndiko kilimo hicho kimepamba moto.

Aidha alitumia nafasi hiyo kuwashauri wakulima wa tumbaku wasikubali kupangiwa ekari za kulima , bali kila mkulima aachwe alime kulingana na uwezo wake.

Ameongeza CCM CCM inafuatilia kwa karibu kwani waliahidi kwenye Ilani ya Uchaguzi na sasa wana kazi ya kufuatilia yale waliyokubaliana yanatekelezwa huku akiwahakikisha na yeyote mwenye nia au dhamira ya kuhujumu jitihada hizo hawatamzama machoni.

“Tuliahidi na leo tunatekeleza , nataka niwaambie siri moja ya CCM kuendelea kubaki madarakani ni namna ambavyo tunaahidi na kutekeleza mbele ya watanzani na hiyo sifa tutaiendeleza kwasababu tunaye kinara, jemedari , mpiganaji lakini tunaye mtu aliyeamua kuyabeba maono yenu ambaye ni Rais Samia na kwa kuwa tunaye jemedari wetu CCM itaendelea kutawala miaka 100 ijayo,”alisema.

Akizungumza Mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini Mheshimiwa Almasi Maige amezungumzia Umuhimu wa Ujenzi wa Kiwanda Cha Tumbaku kujengwa katika Wilaya Hiyo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments