KATIBU MKUU CCM AAGIZA MAENEO YOTE YA HUDUMA ZA KIJAMII YAPIMWE ILI YAWE NA HATI

Chama  Cha Mapinduzi( CCM) kupitia Katibu MKuu wake Daniel Chongolo kimetoa maagizo kwa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI) pamoja na Wizara ya Ardhi kuhakikisha wanaweka utaratibu utakaowezesha halmashauri zote nchini kupima maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya huduma za kijamii.


Lengo la kupima maeneo ni kwa ajili ya kupata nyaraka za umiliki hali wa kisheria ili asije kutokea mtu mjanja akatangaza eneo fulani ni lake na anaweza kuchukua kwasababu tu halmashauri haina hati,hivyo lazima maeneo yote yapimwe na nyaraka zake kuhifadhiwa kwenye halmashauri na kulindwa vizuri.

Akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na Wananchi wa Kata ya Mamsera katika Halmashauri ya Rombo kwenye tarafa ya Mengwe alipokwenda kukagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ambayo haikuwahi kuwepo katika kata hiyo Katibu wa Mkuu Chongolo ametoa mwito kwa kupimwa kwa maeneo yote ambayo yametengwa kwa ajili ya huduma za jamii.

"Mwito wangu na huu nautoa kwa Wizara ya TAMISEMI pamoja na Wizara ya Ardhi lazima sasa tuweke kipaumbele cha kupima maeneo ya huduma nchi nzima,tuwe na hati za maeneo hayo ili yasiingiliwe au yasiwe na migogoro.Hapa mmesema mmechukua eneo kidogo la shule ya msingi na maeneo mengine mmenunua kwa wenyeji.

"Bila kuyapima na kuyaweka kwenye hati ya shule halmashauri wataihifadhi ile hati tutabakia nayo kwani siku moja watoto watakaokuja kusema unajua kihamba yetu ilikuwa inapita mpaka hapa na kwasababu hela amechukua baba na baba hayupo wanaanzisha mgogoro na utasumbua watu tutakaowaachia hapa huko mbeleni.

"Lazima tujenge na tuweke utaratibu utakaohakikisha maeneo yote ya huduma ziwe za shule,afya, Ofis za Serikali na maeneo mengine ya michezo na yaliyohifadhiwa yanapimwa na kuhifadhiwa na kutolewa nyaraka kwa ajili ya uhifadhi ndani ya Mamlaka za Serikali zilizopo maeneo husika.

"Tusipofanya hivyo itafika wakati tutakosa maeneo ya kufanya shughuli za maendeleo, leo zitakuja hapa fedha zingine mkaambiwa zinatakiwa kujengwa kidato cha tano na Sita mtajenga wapi? Maana yake mtakosa fursa kwasabau ardhi ambayo ilitengwa kwa ajili ya huduma hizo si ajabu zikabadilishiwa matumizi,"amesema Chongolo.

Ameongeza ni lazima wawe na uchungu na ardhi ambayo imehifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya watu wote na yalindwe kama mboni ya jicho ili baadae isaidie kuleta matokeo kwenye matumizi yatakayokuwa yakipangwa, hiyo ndio kazi ya watumishi na watendaji wa Serikali.

Chongolo amesema lazima kiongozi wa Serikali aache alama ya kufanya jambo la tofauti."Hatuwezi kuwa na eneo lina miundombinu mizuri na la kisasa lakini tukiuliza nani amiliki eneo hili tunaanza kunyoosha kidole ,ukiambiwa onesha dokumenti huna , hivyo akitokea mjanja atapima na kuchukua hati atatuondoa.

"Na akituondoa miundombinu hii tutakuwa tumepata hasara kwa uzembe wetu wa kutopima maeneo na kuyaweka na kuyamiliki kisheria, lazima Wizara ya TAMISEMI na Wizara ya Ardhi iweke programu ya kuhakikisha maeneo yake yanapimwa na iweke malengo kwa kila Mkurugenzi wa Halmashauri.

"Na Katibu Tawala wa Mkoa kuhakikisha katika kipindi fulani wanayatambua maeneo yote ili wayawekee programu kama yako maeneo 100 waseme kila mwaka maeneo 30 yawe yamepimwa na baada ya miaka mitatu na nusu watakuwa wamepima maeneo yote yatakuwa na nyaraka na mmbo yetu yatakuwa yametunyokea,"amesema

Ameongeza kwamba "Hawawezi kufanya mambo kwa utamaduni wa zamani, sasa hivi wajanja ni wengi wakiona batii inanga'aa na hii kijani yenye matumaini anaanza kuwaza namna gani mambo yatamnyookea, tujajukuta shule zinamilikiwa katika viwanja vya watu binafsi, hivyo lazima maeneo hayo yamilikiwe na Serikali.

"Tunataka hati ikae ofisi ya mtendaji na nakala kubwa ikae kwenye Ofisi ya Halmashauri na tena inapokaa fungua anakuwa nayo Mkurugenzi , Mwenyekiti wa Halmashauri, au inakuwa na password maana siku hizi mambo yanaenda kisasa.Mkurugenzi aweke dole gumba,Mweka Hazina aweke dole gumba na ikiwezekana aje na mtu mwingine anayeaminiwa na Serikali ya Wilaya kuwa yeye ndio dole gumba la mwisho.

"Kama ni Katibu Tawala wa Wilaya au Mkuu wa Usalama wa Wilaya au Mkuu wa Wilaya ndani ya Wilaya husika akiondoka anapewa mtu mwingine na kuweka kidole gumba,hivyo mtakuwa salama kabisa na hakuna mtu anaweza akacheza nazo.Lazima tupime kuhakikisha usalama wa maeneo yetu.Pimeni maeneo mjue mipaka yenu yajulikane."

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiwa pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga na Viongozi wengine wa Chama na Serikali wakitoa heshima mbele ya kaburi la wanafunzi 38 wa shule ya Sekondari ya Shauritanga waliopoteza Maisha yao katika ajali ya moto iliyotokea tarehe 18 Juni 1994.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiweka shada la maua katika kaburi la wanafunzi 38 wa shule ya Sekondari ya Shauritanga waliopoteza Maisha katika ajali ya moto iliyotokea tarehe 18 Juni 1994.




Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akiweka shada la maua katika kaburi la wanafunzi 38 wa shule ya Sekondari ya Shauritanga waliopoteza Maisha yao katika ajali ya moto iliyotokea tarehe 18 Juni 1994







Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiwasili Mamsera, Rombo mkoani Kilimanjaro kujionea maendeleo ya ujenzi wa shule ya Sekondari Mamsera Kati ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua uhai wa Chama pamoja na Kuhimiza na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025. 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiwa akiwa na Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Kilimanjaro wakati alipotembelea mradi ujenzi wa shule ya Sekondari Mamsera Kati ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua uhai wa Chama pamoja na Kuhimiza na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025. 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rombo Ndugu Anthony Joachim Tesha (kushoto) mara baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari Mamsera Kati ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua uhai wa Chama pamoja na Kuhimiza na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025. 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akihutubia wakazi wa Namsera, Rombo mkoani Kilimanjaro mara baada ya kutembelea na kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Mamsera Kati ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua uhai wa Chama pamoja na Kuhimiza na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025. 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Ndugu Nurdin Babu mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari Mamsera Kati ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua uhai wa Chama pamoja na Kuhimiza na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments