Latra: Mabasi yasiyotumia tiketi mtandao mwisho Septemba 1

 Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra), imesema kuanzia Septemba 1, 2022,  mabasi yanayofanya safari za mikoani na nchi za nje yasiyotumia tiketi za mtandao hayaturusiwa kufanya shughuli za usafirishaji wa abiria.

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi Agosti 18, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Habibu Suluo wakati akizungumza na wanahabari kuhusu maendeleo ya mchakato wa matumizi ya tiketi mtandao kwa mabasi yanayoendea katika mikoa mbalimbali na nchi za jirani.

Amesema kipindi cha majaribio ya matumizi ya tiketi mtandao kilikuwa kuanzia Aprili Mosi mwaka huu hadi Juni, lakini Latra ikishirikiana na wadau wakiwamo Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa) walikubaliana kuongeza muda.

"Mamlaka iliongeza muda wa miezi miwili hadi Agosti 31 unaombatana na utoaji wa elimu kuhusu suala hili. Changamoto zilizokuwa zikijitokeza katika mchakato huu zimeshafanyiwa kazi," amesema Suluo.

Kwa mujibu wa Suluo, hadi Agosti 17, 2022 jumla ya mabasi 2,033 kati ya 3,916 yanayomilikiwa na kampuni za usafirishaji wa abiria yaliunganishwa na tiketi mtandao na kubaki 1, 883 sawa asilimia 52.

"Kwa hatua hii hatua mamlaka imepanga kuchukua hatua stahiki ikiwamo kutoa adhabu ya faini au kusitisha huduma ya mabasi yote yatakayoshindwa kutimiza takwa hili ifikapo Septemba Mosi," amesema Suluo.

Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabara, Johansen Kahatano amesema suala la tiketi mtandao ni la kila mtu na lina faida kwa wananchi na Serikali. Amewataka abiria kuwa mstari wa kukata na kudai tiketi mtandao badala ya tiketi za karatasi.

Chanzo Mwananchi

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments