MGUMBA AANZA NA BANDARI TANGA, ASEMA IMECHANGIA MKOA KUONGOZA UKUSANYAJI MAPATO.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba akimsikiliza meneja uendeshaji, katikati ni Meneja wa Kampuni hiyo Mkoa wa Tanga Amour Ally.
Meneja uendeshaji wa Kampuni ya GBP, Fahim Salim akitoa maelezo kwa mkuu wa Mkoa alipotembelea kwenye Kampuni hiyo
kuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba akikagua flowmeter wakati wa ziara hiyo


Meneja wa Bandari Mkoa wa Tanga akitoa maelekezo kwa mkuu wa Mkoa huo Omari Mgumba alipotembelea Bandari hapo kukagua maendeleo ya mradi.



MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba ametangaza fursa kwa wawekezaji wa nje na ndani ya nchi kuja kuwekeza katika Bandari ya Tanga upande wa mahala ya kuhifadhia mizigo.


Mgumba ametoa kauli hiyo wakati alipotembelea Bandari hiyo ikiwa ni moja ya ziara yake kikazi baada ya kukabidhiwa Mkoa huo na kusema ameanza kuzuru katika eneo hilo kutokana na maendeleo mazuri ya mradi uliopo.


Amesema pamoja na upanuzi mkubwa wa kina katika Bandari unaoendelea Kuna shida ya sehemu ya kuhifadhia mizigo kwakuwa kabla ya mradi huo kulikuwa na uhaba wa magala hivyo kwa upanuzi huo kunahitajika eneo zaidi la kuongeza magala.


"Taarifa yenu imesema sehemu ya kuhifadhia mizigo watu wakija hapa hakuna, sasa hii ni shida kwenu lakini ni fursa kwa wawekezaji, kwahiyo wawekezaji popote walipo iwe ndani au nje ya Tanzania, wake kuwekeza Tanga katika maeneo ya uhifadhi wa shehena za mizigo,


"Kwasababu Bandari hii ikikamilisha ule upanuzi, uwezo wake utaongezeka kutoka tani laki saba hadi tani milioni tatu, sasa kama tuna Tani laki saba tunashindwa kuhifadhia ikiwa hiyo milioni tatu tatawezaje kuiweka mizigo inayotoka ndani na nje ya nchi yetu" amesema.


Aidha Mgumba ametoa pongezi kwa Rais na wetandaji katika Mkoa huo kwa kazi nzur ya ukusanyaji wa mapato hususani kwa TRA na jiji huku akibainsha kuwa uwepo wa Bandari hiyo umechangia kwa kiasi kikubwa kuingiza mapato ambayo yameleta tija na kufanikiwa kushika namba moja katika ukusanyaji.


Sambamba na hilo amesema uwekezaji mkubwa wa Bandari hiyo ni lazima uendane sambamba na miundombinu ukiacha ya magala lakini pia ya barabara, hivyo ni lazima kuunganisha Barabara kuu ya Tanga hado Dodoma kupitia Handed, Kilindi kwa kiwango cha lami ili kufunguka milango ya biashara.


"Lakini ni lazima tufungue Barabara kwa kiwango cha lami kwa kasi hii ya ujenzi ambayo inaonekana kupitia Dumila, Morogoro ili tuunganishe Kilosa hadi Mikumi, inakwenda Kilombero mpaka Ruvuma, kwahiyo watu wa Malawi watapata huduma ya Bandari hii kupitia Barabara ya Ruvuma" amesisitiza.


Naye Meneja wa Bandari Mkoa wa Tanga Masoud Athumani amesema mradi huo unaotarajiwa kukabidhiwa Novemba mwaka huu utaweza kuhusumia shehena tani milioni tatu badala ya laki saba za hapo awali kabla ya kina cha Bandari kuongezwa.


Katika ziara yake Mgumba alitembelea Kampuni ya mafuta ya GBP jijini humo na kutaka kujua sababu inayofanya wateja kushindwa kuchukua mafuta Tanga na kwenda kujazana Dar es salaam wakati Tanga mafuta yanapatikana tena bila msongamano wowote na gharama nafuu.
 Chanzo :Sayari News Blog

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments