MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI MIPYA MINNE IKUNGI

 

Muonekano wa mradi wa Tenki kubwa lenye uwezo wa kuhifadhi maji Lita laki moja (100,000) lililojengwa na Kampuni ya Chakwale kwa ufadhili wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassani- ni moja ya miradi iliyokamilika na inatarajiwa kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru wilayani humo kesho kutwa Agosti 13 mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro (katikati) akiwa na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo baada ya kukagua mradi wa maji uliojengwa na Kampuni ya Chakwale kwa ufadhili wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassani ambao utazinduliwa na Mwenge wa Uhuru wilayani humo keshokutwa.

*********************

AGOSTI 13 mwaka huu, ujumbe wa mbio za Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuzindua miradimikubwa ya kiustawi na maendeleo, ikiwemo mradi wa maji kwa wakazi wa vijiji vya Ikungi naUnyahati, daraja la Barabara ya Makiungu-Utaho, nyumba za watumishi na ujenzi wa vyumba vya madarasa ndani ya Wilaya ya Ikungi mkoani hapa.

Ikumbukwe, kasi ya ujenzi wa miradi itakayozinduliwa na Mwenge wa Uhuru ndani ya wilayaya Ikungi ni mwendelezo wa miradi mingine mikubwa inayoendelea kutekelezwa, ikiwemo ujenzi wa chuo kikubwa cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), ujenzi wa Hospitali ya Wilaya,miundombinu ya barabara na vituo vya kutolea huduma za afya-ambayo baadhi yakeilitembelewa na kuwekewa mawe ya msingi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa-hivi karibuni.

Akizungumza wakati akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji wa kijiji cha Ikungi naUnyahati (moja ya mradi unaotarajia kuzinduliwa na Mwenge), Mkuu wa Wilaya hiyo Jerry Muro alisema kasi kubwa ya ujenzi wa miradi unaoendelea kwasasa inachagizwa na dhamira safi na upendo wa hali ya juu wa Rais Samia Suluhu Hasssan kwa wana-Ikungi na wakazi wote wa mkoa wa Singida.

“Natoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais…na niwaombe wakazi wa Ikungi tuzidi kumtiamoyo kwa kumpa ushirikiano katika kipindi hiki ambacho anapambana sana kustawisha uchumi na kuleta matokeo chanya ya hali bora za kihuduma kwenye nyanja zote za kijamii, ikiwemo afya, elimu, maji, na maboresho ya miundombinu ya Barabara kwa wana-Ikungi na taifa kwa jumla.

Aidha, katika kufanikisha azma chanya ya ujio wa Mwenge wa Uhuru, Muro aliwasihi wakaziwote wilayani hapa kujitokeza kwa wingi kuupokea, ambapo pamoja na mambo mengine pia unatarajia kufanya shughuli nyingine-zikiwemo kuzindua Kikosi Maalumu cha Kupambana na Rushwa, kushiriki kushiriki zoezi la upandaji miti, kutembelea na kupokea taarifa ya hali halisi ya ugonjwa wa Maralia kutoka kwenye banda la utoaji elimu lililopo eneo la Puma.

Mabanda menngine yatakayotembelewa eneo hilo ni pamoja na banda la elimu ya UKIMWI/Vvu, dawa za kulevya, lishe, dawati la malalamiko, sensa ya watu na makazi na mradiwa vijana (Tehama) kabla ya kuelekea eneo la Issuna Madukani kwa ajili ya mkesha.

Imeelezwa, kulingana na ratiba baada ya mwenge kupokelewa alfajiri eneo la Njiapanda wilayani hapa utapita kwenye maeneo kadhaa kulingana shughuli zilizoorodheshwa kiitifaki,ikiwemo maeneo ya Shule za Sekondari Siuyu na Issuna, Minyinga, Puma, Ikungi na kishaviwanja vya Issuna Madukani kwa ajili ya risala ya utii na ujumbe mahsusi wa Mwenge, kabla ya kuelekea Kijiji cha Gurungu (Itigi) mapema Agosti 14 kwa makabidhiano.
Na Godwin Myovela, Ikungi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments