PITSO MOSIMANE: YOUNG AFRCANS INAFANYA MAMBO YAKE KISASAAliyekuwa kocha wa klabu ya Al Ahly ya nchini Misri Pitso Mosimane amesema kuwa ameamua kushiriki Siku ya kilele cha Mwananchi kwasababu ni muda wake sasa wakuwa mapumziko kwani amekuwa uwanjani kwa muda mrefu kwenye mechi za mashindano.

Ameyasema hayo leo mara baada ya kuwasili nchini kwaajili yakushiriki Wiki ya Mwananchi ambapo kilele ni hapo kesho Agosti 6.

"Nilikuwa Uwanjani kila siku na mechi za mashindano zikiwa kila baada ya siku 3 na nilikuwa nasafiri sana, Sasa nimeamua kupumzika na mapumziko yangu nayatumia kushiriki na Young Africans Sc katika Wiki Ya Wananchi" . Amesema

Amesema Afrika inatakiwa kujipanga katikakuhakikisha soka linakuwa hasa kwa kuendeleza vijana wenye vipaji vya soka wakiwa bado wadogo ili baada waweze kufanya makubwa .

"Nikiwa kama Kocha kutoka Afrika nimefanya makubwa kwenye soka la Afrika na nina amini Afrika tuna nafasi ya kufanya zaidi ya nilichokifanya kwenye soka kukuza Mpira wetu ulimwenguni kote" Amesema Pitso Mosimane

Aidha amesema kuwa alifurahishwa na shangwe za mashabiki wakati wakipokea kombe na kufanya sherehe za aina yake hivyo imekuwa yakuvutia.

"Niliona hamasa kubwa ya mpira kwenye Sherehe za Ubingwa (parade) kwa Mashabiki wa Klabu hii pendwa na hamasa hii ilipelekea Dunia nzima kuangalia kile walichofanya Yanga kwenye mapokezi ya Ubingwa na ilinivutia kupita kiasi" Ameeleza

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments