RC SERUKAMBA ATUA IKUNGI UKAGUZI SENSA

 Mkuu wa mkoa wa singida Mhe. Peter Serukamba ameridhishwa na jinsi wilaya ya ikungi inayoendesha zoezi la sensa ya watu na makazi kwa mwaka 2022 na kuitaka wilaya leo jumamosi tarehe 27/08/2022 wamalize zoezi lote la sensa ya watu na makazi 

Rc Serukamba amesema kama mpaka sasa wilaya imeshafikisha zaidi ya asilimia 85 kwa kuandikisha kaya zaidi ya elfu 51 kuna uwezokano mkubwa wakamaliza zoezi hilo mapema iwezekanavyo

Wakati huo huo Rc Serukamba amewataka wasimamizi na waratibu wa sensa ikungi kuwahamisha makarani waliomaliza katika maeneo yao na kuwapeleka kwenda kuongeza nguvu katika maeneo ambayo hayajafikiwa na yana idadi kubwa ya kaya uku zingine zikiwa kwenye umbali kufikiwa 

Mkurugenzi wa halmashauri ya Ikungi Ndugu Justice Kijazi amemuhakikishia Rc Serukamba kuwa zoezi litakwen itda vizuri na litamalizika katika muda uliopangwa na kwa uadilifu mkubwa.








TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments