Uamuzi huo umetangazwa leo, Waziri wa Elimu, George Magoha baada ya kuwapo kwa mijadala juu ya shule hizo kufunguliwa kesho wakati mpaka saba bado shughuli hiyo inaendelea huku baadhi ya maeneo wakazi wake hawajapiga kura.
Fuatilia matokeo uchaguzi mkuu Kenya hapa
Baadhi ya walimu, wazazi, walezi na wanafunzi walipinga uamuzi wa awali wa wizara hiyo kufungua shule Agosti 11 baada ya kuzifunga Agosti 5 kwakuwa shule hizo ndizo zinazotumika kama vituo vya kupigia na kuhesabu kura hivyo walihitaji muda zaidi wa wanafunzi kusalia nyumbani.
Hata hivyo leo, Waziri Magoha ameeleza "Baada ya mashauriano, natangaza uamuzi wa Serikali kwamba taasisi za elimu ya msingi zitafunguliwa kuanzia Jumatatu (Agosti 15, 2022)”.
0 Comments