Ushirikiano Baina ya
walimu wa michezo, wakuu wa shule na maafisa elimu, Michezo Na Vyama Vya
Michezo umeiwezesha Halmashauri ya Manispaa
Ya Singida kuibuka mshindi wa jumla
katika mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISETA) Ngazi
ya Mkoa wa Singida Ikizoa vikombe Vinne vya mshindi wa kwanza katika michezo
mbalimbali.
Kauli hiyo ilitolewa Na Afisa Elimu Mkoani Singida Maria Lyimo, alipokua akiongelea siri ya mafanikio ya Michezo
Mkoani Singida katika
kilele cha michezo ya UMISETA ngazi ya Mkoa iliyofanyika Katika viwanja vya
shule ya sekondari Mwenge.
Afisa Elimu Mkoa Wa Singida Maria Lyimo Limo alisema “Mkoa Wa Singida tumejipanga
vizuri. Mara tu baada ya kumaliza Mashindano ya mwaka jana. Tulianza mikakati
mapema kuanzia ngazi ya shule, tarafa na wilaya”.
Mkuu huyo wa Idara ya Elimu Sekondari alisema kuwa
ushirikiano mkubwa baina ya walimu wa michezo, wakuu wa shule na maafisa Kwa Kupitia Mwenyekiti Wa Chama Cha Mpira Wa Miguu
Na Mwenyekiti Wa Kamati Ya Michezo Mkoa Wa Singida Bw Hamis Kitila ndiyo siri
kubwa ya mafanikio kwa timu ya (UMISETA) ya Mkoa Wa Singida kufanya vizuri. “Wakati wa kufanya uchaguzi wa
wanamichezo Tulikuwa Na umakini mkubwa. Tuliwachagua kwa uwezo wao na siyo kwa
upendeleo. Tuliwatumia Waamuzi wa Nje wenye sifa kuchezesha na kufanya uchaguzi
makini wa wanamichezo kwa lengo la Kujenga timu Imara na itakayotoa ushindani na
kulinda hadhi ya Mkoa Wa Singida.
Kwa Upande Wa Mwenyekiti Wa Kamati Ya Michezo Mkoa Wa
Singida Bw. Hamisi Kitila alisema kuwa Mkoa wa Wa Singida una imani kubwa na timu hiyo ya mkoa. “Sisi
viongozi wa mkoa hatuna maneno Mengi ya kusema, mengi mmeshaambiwa na viongozi
wenu. Zingatieni taratibu za michezo hii, kwa jinsi Nilivyowaona hapa nidhamu
imetamalaki. Mkoa tunawatakia ushindi mkubwa, mlete.
Afisa Michezo Mkoa Wa Singida Mwalim Amani Mwaipaja Amewashukulu Wadau Wote
Walijitokeza Katika Kuwezesha Michezo Kufanyika Na Kumalizika Salama Kwa Ngazi
Ya Mkoa Na Kupata Timu Ya Wanamichezo 120 Watakao Wakilisha Mkoa Katika
Mashindano Ya (UMISETA) Kitaifa Yatakayofanyika Mkoani Tabora.
Tazama Picha Mbali Mbali Za Matukio Katika Ufungaji Wa Mashindano Ya (UMISETA) Nganzi Ya Mkoa Singida.




























Na Abdul Bandola Ramadhani:Singida.
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI
Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516
0 Comments