WAZIRI MKUU AWASILI TUNISIA KUHUDHURIA MKUTANO WA TICAD

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasili Tunisia leo (Ijumaa Agosti 26, 2022) na kupokelewa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mhe. Najla Bouden Romdhane katika uwanja wa ndege wa Carthage, jijini Tunis.


Waziri Mkuu anatarajiwa kumwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa TICAD ambao unaanza kesho Jumamosi, Agosti 27, 2022.


Katika mazungumzo yao uwanjani hapo, Waziri Mkuu alipata wasaa wa kubadilishana mawazo na mwenyeji wake ambapo walijadiliana masuala kadhaa kuhusu demokrasia na utawala bora, uhusiano wa kimataifa na uchumi.


Mkutano huo utakaofanyika Agosti 27-28, 2022 unatoa fursa ya kupanga mikakati ya ushirikiano na ajenda za kimaendeleo zitakazotekelezwa kati ya Japan na Afrika. Rais wa Senegal, Mhe. Macky Sall na Waziri Mkuu wa Japan, Mhe. Kishida Fumio watatoa hotuba za ufunguzi wa mkutano huo.


Tanzania imekuwa ikishiriki mikutano hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993. Kufuatia mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Japan hususani kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Tanzania imekuwa ikinufaika na utekelezaji wa miradi mbalimbali katika sekta za miundombinu ya barabara, nishati ya umeme, maji, elimu, afya na kilimo.
Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, akisalimiana na Waziri Mkuu wa Tunisia Mhe. Najla Bouden Romdhanemara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Carthage, jijini Tunis, Leo 26 Agosti 2022. , Waziri Mkuu anatarajiwa kumwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa TICAD ambao unaanza kesho Jumamosi, Agosti 27, 2022.

Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, akiongozana na Waziri Mkuu wa Tunisia Mhe. Najla Bouden Romdhane mara baada ya kumpokea katika uwanja wa ndege wa Carthage, jijini Tunis 26 Agosti 2022. , Waziri Mkuu anatarajiwa kumwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa TICAD ambao unaanza kesho Jumamosi, Agosti 27, 2022.
Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, akizungumza na Waziri Mkuu wa Tunisia Mhe. Najla Bouden Romdhane mara baada ya kupokelewa katika uwanja wa ndege wa Carthage, jijini Tunis Leo 26 Agosti 2022., Waziri Mkuu anatarajiwa kumwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa TICAD ambao unaanza kesho Jumamosi, Agosti 27, 2022.
Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, akiagana na Meya wa Jiji la Tunis Mhe. Souad Abderrahim, mara baada ya kupokelewa na kufanya mazungumzo katika uwanja wa ndege wa Carthage, 26 Agosti 2022. Kulia ni Waziri Mkuu wa Tunisia Mhe. Najla Bouden Romdhane (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments