DC IKUNGI ATAKELEZA MAAGIZO YA WAZIRI MKUU MAJALIWA

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C. Muro ameendelea na zoezi la utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu Mhe. Kasim Majaliwa Majaliwa ya kumaliza migogoro sugu ya ardhi kwa baadhi ya wananchi wilaya ya Ikungi

Katika utekelezaji wa maagizo hayo, Dc Muro mara baada ya kushughulikia changamoto hizo sasa amekutana nankufanya mazungumzo na familia ya Mama amina mohamed mghenyi wa kitongoji cha taru kijiji cha Mang'onyi kata Mang'onyi jimbo la singida mashariki kumuomba aridhie kupokea fidia ya kupisha uendelezaji wa eneo la mradi wa ujenzi wa mgodi mpya wa dhahabu wa shanta mradi wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 80

Katika kikao hicho Dc Muro amelazimika kukutana nae kwa mara ya pili kwa lengo la kumueleza mchakato ulivyofanywa na wathamini wa serikali na vyombo na taasisi za serikali na gharama ya fidia kutengenezwa kwa utaratibu wa kisheria na nyongeza ya hela kidogo kutoka kwa mwekezaji na kumueleza wenzake zaidi ya 25 wameridhia na kupokea fidia zao zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 215 pamoja na kujengwa nyumba mpya za kisasa zenye jiko bora la kisasa

Katika mazungumzo hayo Dc Muro ambae ameambatana na wataalamu wa idara ya ardhi halmashauri ya Ikungi, diwani wa kata husika, na viongozi wa vijiji pamoja na watendaji wa mgodi wa shanta walifafanua na kujibu maswali na hoja zote japo aliweka msisitizo wa kugoma kuridhia kupokea

Katika hatua hii, Dc Muro amemshukuru Mungu kwa mazungumzo kwenda vizuri japo kazi ni ngumu ya kumwelewesha mtu asietaka kuelewa ukweli na kuagiza katika kikao kijacho mwanasheria wa mama amina awepo wafikie muafaka japo ana mamlaka ya kuendelea ila ameona watumie busara zaidi ya kumsikiliza tena na tena tufike muafa

Kazi inaendelea na muda sio mrefu tutafikia muafaka na uwekezaji utaendelea katika eneo la ujenzi wa uwanja mdogo wa ndege na njia ya kupitishia umeme mkubwa kwenda mgodi

*Imetolewa na ofisi ya mkuu wa wilaya Ikungi .14/09/2022*
 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments