Diwani Wa Zamani Chadema ashinda UWT, Mpinzani Wake asema...

Wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) wamelazimika kurudia kupiga kura kumpata mwenyekiti wa umoja huo.

Hatua hiyo imetokana na mgombea aliyekuwa akitetea nafasi hiyo, Agnes Sai kutoridhika na kuamini kuwa amepata kura 79 huku mpizani wake wa karibu, Julieth  Dibaze akipata kura 126 kati ya wagombea wanne.

Uchaguzo huo imefanyika Jumamosi ya Septemba 24, 2022 na kusimamiwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Said Nkumba.

Nkumba amesema awali kura zilizopigwa 256 na kura 2 ziliihalibika kura halali 254 na kufanya matokeo ya awamu ya kwanza kwa wagombea Asha Ramadhani amepata kura11, Abiba Marushwa amepata kura 38.

 Agnes Sai amepata kura 79, huku Julieth Dibaze akipata kura 126 hali ambayo ilimfanya msimamzi kurudia upigaji wa kura baada ya kuridhia wagombea wawili waachiwe munyukano.

"Hu ni murudio wa mwisho kama kupiga kura wagombea ridhikeni na matokeo ya wajumbe," amesema Nkumba.

Bada ya wajumbe kupiga kura kwa mara ya pili, amemtangaza Julieth Dibaze kuwa mwenyekiti mpya wa UWT wilaya ya Bukombe kwa kupata kura 157 huku Agnes aliyekuwa akitetea akiambulia kura 97 ikiwa kura halali zilikuwa 254.

Julieth amechukua nafasi hiyo na amewahi  kuwa diwani viti malumu  2010 hadi 2015 kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na uchaguzi wa 2020 aligombea Udiwani viti malumu kupita CCM kura hazikutosha.

Dibaze akiwashukuru wanawake kwa kumuamini amesema ameamini wanawake wanaweza.

"Nawaahidi kufanya kazi kwa ushirikiano kwa kuimarisha jumuia kwa masilahi ya chama," amesema Dibaze.

Agnes ambaye alishindwa kutetea nafasi yake alisema amepokea matokeo bila kinyongo.

"Asiyekubari kushindwa simshindani nawahakikishia wajumbe naenda kujipanga awamu nyingine na mjue sijachukia mtu," amesema Sai.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments