HATIMAE FAMILIA YA MAMA AMINA MOHAMED MUGHENYI YAPOKEA HUNDI YA FIDIA SHANTA

Familia ya Mama amina mohamed mghenyi wa kitongoji cha taru kijiji cha Mang'onyi kata Mang'onyi jimbo la singida mashariki wamefikia muafa na ofisi ya Mkuu wa wilaya kwa kuridhia kupokea hundi ya fedha ikiwa ni fidia ya malipo ya eneo lao ambalo limechukulia na kampuni ya mgodi wa dhahabu ya Shanta kwa ajili ya upanuzi wa mgodi huo

Akizungumza mara baada ya kupokea hundi Bi. Amina Mohamed Mughenyi amesema ameridhishwa na mchakato w tathmini na kiwango alicholipwa mara baada ya kueleweshwa kwa kina na vielelezo na yeye kupata muda wa kushauriana na familia yake na hatimae kukubali kupokea hundi hiyo

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C. Muro ameshukuru kuona mazungumzo aliyoyasimamia kwa zaidi ya miezi kadhaa yamefikia mwisho kwa pande zote kuridhiana hatua ambayo amesisitiza imeongeza ushirikiano baina ya mwekezaji na wananchi wanaozunguka mgodi 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments