KATAMBI- MFUKO WA MAENDELEO YA VIJANA UMEANZA KUTOA MIKOPO KWA KIJANA MMOJA MMOJA

 Naibu Waziri- Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amesema kuwa serikali imeendelea kufanya jitihada za kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kuweza kujikwamua kiuchumi kwa kutoa mikopo kwa kijana mmoja mmoja na si kwa makundi kama ilivyokuwa awali.


Amebainisha hayo wakati wa ufunguzi wa Mdahalo wa Vijana Kuhusu Upatikanaji wa Mitaji na Kukuza Shughuli za Kilimo Biashara kwa Vijana, tarehe 15 Septemba, 2022 Dodoma. Ameongeza kuwa muongozo mpya uliotolewa umerahisisha sifa za kukopa kwa vijana kulingana na mahitaji yao.

Naibu Waziri Katambi amefafanua kuwa yapo maboresho ya mifumo katika kila sekta zinazoshughulikia masuala ya vijana ambapo mifumo hiyo itasaidia kuleta mazingira wezeshi kwa vijana kuweza kujikwamua kiuchumi na kuweza kujiajiri.

Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kushirikiana na Sekta Binafsi katika kutoa mafunzo kwa vijana ili kuweza kutatua changamoto za kiuchumi kwa vijana, Aidha amesisitiza kuwa mafunzo hayo yanasaidia kuongeza maarifa,ujuzi na mipango thabiti kwa vijana kuweza kutambua vipaji vyao.

“Tunafurahi kwamba leo katika mdahalo huu ulio tolewa na shirika AMDT (AGRICATURAL MARKERT DEVELOPMENT TRUST) imetupa fursa ingine ya kusikiliza changamoto, vipaumbele, uzoefu na matarajio toka kwa vijana wote wa kike na kiume.wanaofanya shughuli zao za kiuchumi katika sekta ya kilimo.

Amesisitiza kuwa vijana waliopata mafunzo hayo waendelee kushirikiana na vijana wengine ili kubadili mitazamo na kushirikiana na Serikali kukabiliana na changamoto zinazo wakabili.

Naibu Waziri- Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akizungumza jambo wakati ufunguzi wa Mdahalo wa Vijana Kuhusu Upatikanaji wa Mitaji na Kukuza Shughuli za Kilimo Biashara kwa Vijana, tarehe 15 Septemba, 2022 katika ukumbi uliopo Morena Hotel jijini Dodoma.

Sehemu ya vijana waliohudhuria Mdahalo ulioandaliwa na shirika AMDT Kuhusu Upatikanaji wa Mitaji na Kukuza Shughuli za Kilimo Biashara kwa Vijana, tarehe 15 Septemba, 2022 katika ukumbi uliopo Morena Hotel jijini Dodoma.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments