KINANA AISHUKURU SERIKALI YA CHINA KUFANIKISHA UJENZI WA VETA KAGERA

 MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana ameishukuru serikali ya China kwa kufanikisha ujenzi wa Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) mkoani Kagera.

Mradi huo umegharimu Sh.bilioni 22 bila kodi ya ongezeko la thamani(VAT) ikijumuisha shughuli za ujenzi , usimamizi na uwekaji wa vifaa vya kujifunzia , mashine na samani.

Akizungumza leo Septemba 2, 2022 baada ya kukagua Chuo hicho cha VETA Mkoa wa Kagera, Kinana amesema  anatoa shukrani kwa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa kufanikisha ujenzi huo itasaidia Watanzania wengi kuelimika.

Aidha amewapongeza wananchi wa Bulugo kwa kutoa ardhi na ni matumaini yake kwamba nao watakuwa sehemu ya wanafunzi watakaosoma hapo.

“Nataka nichukue nafasi hii kuipongeza Serikali kwa kazi nzuri inayofanya chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan , katika sekta zote , ninyi ni mashahidi tangu Rais ameingia madarakani shule nyingi zimejengwa, vyuo vingi vimejengwa na walimu wameajiriwa na wanafunzi wameongezeka," amesema na kuongeza kuwa

“Nina hakika watanzania wengi wataelimika kwa hiyo nampongeza Rais kwa kazi nzuri anayofanya.Nichukue nafasi hii kuwashukuru wananchi wa Jamhuri ya Watu wa China , niishukuru Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China , niseme bila kusita tunao marafiki wengi .

Katika hatua nyingine Kinana amekutana na kuzungumza na wanachama wa CCM Mkoa wa Kagera na kuwakumbusha viongozi kuwajibika kwa kuwatumikia wananchi na kusikiliza changamoto zao na kuzipatia ufumbuzi.

Aidha, ametumia nafasi hiyo kutoa maelekezo kwa viongozi wa mkoa huo kuhakikisha wanatatua changamoto za wananchi ikiwemo ya uuzaji wa kahawa baada ya kupokea malalamiko ya wakulima wa zao hilo kusumbuliwa na baadhi ya viongozi.

Kinana  ameshauri wakulima wa zao la kahawa waachwe wauze kahawa yao kokote wanakotaka ilimradi bei iwe nzuri.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments