MAKAMU MWENYEKITI CCM ARIDHISHWA NA UJENZI WA MELI YA MV MWANZA

  AKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amesema ujenzi wa Meli ya MV Mwanza unakwenda vizuri na anatamani kuwa miongoni mwa watu wa kwanza watakaiopanda baada ya ujenzi wake kukamilika.


Akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 jijini mwanza leo Septemba 5, 2022, Kanali Kinana pqmoja na mambo mengine ametembelea eneo inapojengwa meli hiyo na kueleza ameona hatua kubwa imepigwa

"Hongereni ndugu wafanyakazi kwa kazi kubwa na nzuri mnayoifanya ya kuijenga meli hii na ikikamilika mimi nitakuwa wa kwanza kuja kupanda," amesema akiwa katika eneo hilo ambapo ujenzi wa meli hiyo ambao umefika asilimia 70.

Awali akielezea maendeleo ya ujenzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MCSL) Erick Hamisi, amesema meli hiyo yote imeshaunganishwa na ujenzi umefika asilimia 71.

"Block zimeshaunganishwa na kwa taarifa tu blocks hizi zilikuja na ukubwa huu kutoka Korea Kusini...uunganishaji wote umefanyikia hapa na Watanzania 200 wamenufaika na mradi huu .Uchomeleaji wake umekuwa wa kisasa.

"Ujenzi wa meli hii ulitakiwa ukamilike ndani ya miaka miwili lakini chelezo ndio ilichelewa Kukamilika kwani ilikuwa chelezo ianze lakini vilienda pamoja, mradi huu wote unafanyika hapa hapa kwa hiyo tumepata teknolojia mpya. Sasa hivi hatua tuliyofikia na hii meli imebaki kuizindua, kuiweka majini, kuipaka rangi na mwisho wa mwezi wa 10 itaingia kwenye maji, hii ni hatua kubwa sana kwa ujenzi wa meli.

"Itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200, tani 400 za mizigo na magari 23 makubwa matatu na madogo 20. Meli ni kubwa ina urefu wa mita 92.6, uwanja wa mpira wastan una mita 100, kwa hiyo ni mita 100 toa 92.6, ina urefu wa mita 20 karibu ghorofa nne, amesema.

Pia ina upana wa mita 17, ni meli kubwa kuliko meli zote zilizowahi kuelea katika maziwa makuu nchini. Hakuna meli kama hii Kenya, Uganda wa nchi nyingine na hii meli itakuwa na madaraja sita tofauti likiwemo la VIP, itakuwa na uwezo wa kwenda Bukoba kwa saa saba tu tofauti na sasa ambazo hutumia saa 10 hadi 14, kwa hiyo huu ni ukombozi mkubwa," amesema.

Aidha, amesema meli hiyo itakuwa ikifanya safari nje ya Tanzania katika mataifa ya Uganda na Kusumi (Kenya).
Muonekano wa Mv Mwanza ikiendelea kujengwa kando kando ya ziwa Victoria mkoani Mwanza
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akipata maelezo kuhusu ujenzi wa Meli ya MV Mwanza kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MCSL) Erick Hamis Septemba 5,2022 jijini Mwanza, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025. 

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mbunge wa Ilemela Dkt Angelina Mabula ambaye pia ni Waziri wa Ardhi mara baada ya kukagua ujenzi wa Meli ya MV Mwanza Septemba 5,2022, jijini Mwanza, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akisalimiana na baadhi ya wajenzi wa Meli ya MV Mwanza jijini Mwanza, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 mkoani humo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments