Samia akabidhi vifaa tiba

Wakati Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ikichanganua fedha za Uviko-19, Sh203.14 bilioni zilivyotumika, Rais Samia Suluhu Hassan amekabidhi vifaa tiba vilivyonunuliwa kutokana na sehemu ya fedha hizo.

Hayo yamefanyika leo Ijumaa Septemba 30, 2022 wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa usimamizi wa shughuli za lishe.

Akitoa maelezo, Naibu Katibu Mkuu wa Tamisemi, Dk Grace Maghembe amesema walipokea Sh203.14 bilioni ambapo sehemu ya fedha hizo zilitumika katika ujenzi wa majengo ya dharura yaliyojengwa katika halmashauri 80 nchini.

Amesema vigezo vilivyoangaliwa katika kuchagua maeneo ya kujenga ni wingi wa magonjwa ya dharura, umbali wa upatikanaji wa huduma.

Amesema vyumba vya wagonjwa mahututi (ICU) 26 vimejengwa, kutengeneza mitambo ya kuzalishia gesi 20, vifaa vya upasuaji taa na vitanda na vifaa vyake, vifaa tiba mchanganyiko vyote 184.

Dk Grace amesema pia wamenunua machine za mionzi (X-Ray) 137 ambazo zitakwenda katika hospitali zote za wilaya zilizokuwa hazina mashine hizo.

Amesema mashine za mionzi zitakazobakia zitakwenda kuwekwa katika vituo vyote vyenye wagonjwa wengi vikiwemo barabarani ambapo watu wengi wamekuwa wakipoteza maisha.

Awali Katibu Mkuu wa Tamisemi, Profesa Riziki Shemdoe amesema hafla ya kutiliana saini kwa Serikali na wakuu wa mikoa kwa lengo la kuimarisha masuala ya kupunguza matatizo ya lishe ni ya sita tangu utaratibu huyo uanze.

Amesema katika hafla hiyo, pia Rais Samia Suluhu Hassan atazindua magari 52 kati ya 200 kwa ajili ya maofisa elimu sekondari.

Pia atagawa pikipiki 517 kwa ajili ya kufuatilia lishe na vifaa tiba kwa ajili ya zahanati na vituo vya Serikali za mitaa.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema changamoto iliyopo nchini sasa ni watu kutokuwa na uelewa wa lishe.

 “Dodoma mwaka 2018 wakati tathimini inafanyika ilikuwa chini lakini naamini kuwa tathimini ikifanyika sasa hivi itakuwa imepanda,”amesema Senyamule.

 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments