SGR YAKAMILIKA KWA ASILIMIA 90, WABUNGE WASAFIRI KUTOKA DODOMA, DAR WAJIONEA KAZI IKIENDELEA

Ziara  ya ukaguzi wa reli ya kisasa (SGR) ambapo wabunge wa kamati ya miundombinu pamoja na kamati ya uwekezaji na mitaji ya umma (PIC) wametembea na treni ya mkandarasi wa mradi kwa kuanzia stesheni ya Dodoma kuelekea Dar es salam na kushuhudia namna mradi huo ulipofikia.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti wabunge hao wamesema wamefurahishwa na ziara hiyo kwani wamejionea kwa macho yao hatua iliyofikiwa na Serikali katika mradi huo

"Ni safari ya kwanza kwa kwel katika mradi huu na umetekelezeka zaidi ya asilimia 90 kwa hiyo tunaamini mda si mrefu mradi unaenda kukamilika na kuanza na tunajisikia fahari hivyo tuendelee kuiunga mkono Serikali ili iendelee kutekeleza miradi mingine mikubwa zaidi kwa maendeleo na ustawi wa Taifa letu. Sisi kama wabunge tunaowakilisha wananchi maendeleo tumeyaona na kazi kubwa inafanyika" Mbunge Bahati Ndingo.

"Hakika nimejionea kazi zikiendelea kwa kiwango kikubwa sana na zimekamilika kwa asilimia kubwa na kwa kiwango kikubwa hakika mama Samia anatekeleza miradi yote aliyoikuta toka kwa mtangulizi wake kwa kiwango cha spidi kubwa mno na hii reli ni miongoni mwa alama kubwa ambazo yeye binafsi atakuwa ameshiriki wakati akiwa makamu wa Rais na sasa Rais kazi inaendelea na Watanzania tuendelee kuwa pamoja kuyaona mazuri yanayofanywa na Rais wetu na tuunge juhudi mazuri yote anayoyafanya" -Mbunge Viti maalum Mkoa wa Tanga Mwanaisha Ulenge.

"Kwa kweli kazi iliyofanyika ni kubwa sana na wananchi wa Tanzania wana la kujivunia na tumshukuru Rais wetu kwa anayoyafanya na tumtie moyo, Watanzania na tuimbe wimbo mmoja kuwa kazi inafanyika" - Mbunge wa Temeke Mh Dorothy Kilave

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu Mh. seleman Kakoso ameishauri Serikali kuendelea kuimarisha ulinzi wa miundombinu pamoja na kushirikiana na nchi zilizopakana na Tanzania ili kupanua fursa za kibiashara.

"Tunaiomba Serikali wafanye jitihada za kuunganisha Mataifa ya jirani ambayo ni washirika kwenye jumuiya ya Afrika mashariki hasa nchi ya DRC Kongo ambako kuna mzigo mkubwa kwa sana na tunajua DRC Kongo miundombinu ya kwao haiko vizuri" - Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu Mh. Seleman Kakoso.

Pia Mwenyekiti huyo Mh Kakoso amesema jitihada zilizofanywa kupitia TRC ambao ndiyo wasimamizi wanaojenga reli hiyo ki msingi wamerishishwa na jitihada zilizofanywa na Serikali kwa kuwa kila mahala wameona kazi zinavyofanywa katika ujenzi huo wa reli ya kisasa.

"Napenda kuwathibitishia watanzania kuwa reli hii imejengwa kwa kiwango kizuri sana na vimebaki vitu vidogo vidogo sana ambavyo viko kwenye hatua ya mwisho kukamilika na tunaipongeza Serikali na tunawapongeza wafanyakazi wa shirika hili kwa usimamizi mzuri ambao wameufanya na tunaamini Serikali itakamilisha na vipande vingine vya reli ni kiu ya Watanzania kwani kukamilika kwa reli hii kutasaidia sana shughuli za maendeleo kwa Watanzania na gharama za usafirishaji zitapungua na pia gharama za maisha kushuka kwa kiwango cha chini sana"- Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu Mh Seleman Kakoso.

Akizungumzia maendeleo ya mradi wa ujenzi huo Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Reli Nchini (TRC) Mhandisi Masanja Kadogosa amebainisha kuwa Serikali imekuwa ikiendelea kutoa fedha kwa ajili ya kukamilisha mradi huo kwa wakati.

"Ujenzi unaendelea vizuri sana na kwa mara ya kwanza tumeunganisha kutoka Dodoma Dar es salaam na tunaenda na treni ya SGR, najua ni vizuri tumshukuru Rais Samia kwa sababu wakati anahutubia Bunge Mwaka jana mwezi wa nne aliwaahidi Watanzania kuwa ataendeleza miradi ya kimkakati aliyoikuta na wakati anaingia madarakani alikuta tuna vipande viwili, kipande cha kwanza tulikuwa asilimia themanini na cha pili asilimia sitini kwa sasa vipande vyote unaweza kutoka na treni dar es salaam mpaka Dodoma" -Mkurugenzi wa Shirika la rel Nchini Mhandisi Masanja Kadogosa


Wabunge wa kamati ya miundombinu pamoja na kamati ya uwekezaji na mitaji ya Umma (PIC) wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu Mh Seleman Kakoso pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Reli Nchini Mhandisi Masanja Kadogosa, wafanyakazi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka dodoma mpaka Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la Reli Nchini Mhandisi Masanja Kadogosa wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
 Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu Mh Seleman Kakoso akizungumza wakati walipofanya safari kutoka Dodoma hadi Dar es Salaaam kwa kutumia reli ya kisasa (SGR).
Na Janeth Raphael - Michuzi

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments