UVCCM MANYARA WAPATA VIONGOZI WAPYA WA WILAYA

 

Mkoa wa Manyara umepata viongozi wapya wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wa Wilaya sita za Mkoa huo.

Katibu wa UVCCM Mkoa wa Manyara, Ibrahim Kandumila akizungumza mjini Babati amesema uchaguzi huo umekamilika kwa asilimia 100 na kufanyika kwa amani.

Amewataja wenyeviti hao waliochaguliwa na wilaya zao kwenye mabano ni Solomon Mekiory (Babati vijijini), Justin Ammi (Hanang') na Magdalena Urono (Babati mjini).

Amewataja wengine ni Hamza Mngia (Kiteto), Timothy Mollel (Simanjiro) na Elisante Michael (Mbulu).

"Nawapongeza na kuwashukuru wote walioshinda ila watimize majukumu yao ipasavyo na ambao kura hazikitosha wawape ushirikiano wale walioshinda," amesema Kandumila.

Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Babati Vijijini Solomon Melkiory amewashukuru wajumbe wa jumuiya hiyo kwa kumchagua ili awaongoze na ameomba ushirikiano kwao.

Mwandishi wa kituo cha FM Manyara na AYO TV, Charles Mangwe ambaye ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Babati Vijijini kupitia UVCCM amewashukuru wajumbe kwa kumpa kura za ushindi.

Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Babati mjini kupitia UVCCM Husna Mdinku ameomba ushirikiano kwa wajumbe hao na kuahidi kuwaunganisha kupitia nafasi hiyo.

Mjumbe wa mkutano mkuu wa UVCCM Wilaya ya Babati mjini Elias Ernest ambaye ni mwandishi wa kituo cha Wasafi amewashukuru wajumbe kwa kumpatia nafasi hiyo.
Michuzi Blog

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments