Recent-Post

WAZEE IKUNGI WAKUTANA

Ikiwa ni siku moja kabla ya maadhimisho ya siku ya wazee Duniani ambayo kimkoa maadhimisho yatafanyika katika wilaya ya Ikungi, baadhi ya wazee wamekutana na Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C. Muro ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya maadhimisho yatakayifanyika kesho tarehe 01/10/2022

Wakizungumza ofisini kwa Dc Muro wazee hao wameishukuru serikali ya wilaya kwa namna inavyoshughulikia kero na changamoto zinazowakumba wazee na kumuhakikisha Dc Muro kuwa kesho wana jambo la kusema kwa Mheshimiwa Rais. Samia Suluhu Hassan

Katika mazungumzo hayo Dc Muro amewahakikisha wazee kuwa serikali itaendelea kuondoa kero na changamoto zinazowakumba wazee ikiwemo kuweka mfumo endelevu wa kuhakikisha mabaraza ya wazee kuanzia ngazi ya wilaya, kata na vijijini yanafanya kazi ipasavyo hatua itakayowawezesha wazee wenyewe kutatua changamoto ndogondogo zinazowakabili wakati serikali ikiendelea kutatua kero mtambuka za wazee 

Post a Comment

0 Comments