YANGA SC YAICHAPA MTIBWA SUGAR MABAO 3-0, AZIZ KI ATUPIA

 


KLABU ya Yanga imefanikiwa kuondoka na alama tatu mara baada ya kufanikiwa kuichapa Mtibwa Sugar kwa mbao 3-0, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini dar es Salaam.

Mabao ya Yanga yaliwekwa kimyani na mshambuliaji Fiston Mayele, Djuma Shaban pamoja na Azizi Ki ambaye alifunga idadi ya mabao kwenye mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake.

Yanga sasa iitakuwa inaongoza ligi ya NBC kwa kufanikiwa kucheza mechi nne na kujikusanyia pointi 10 akifuatiwa na Azam Fc ambaye amecheza mechi nne na kujikusanyia pointi 8 wakati Simba, Namungo pamoja na Singida Big Star. wakiwa wamecheza mechi tatuu na kujikusanyia pointi 7

Post a Comment

0 Comments