MGODI WA BUCKREEF WASHIRIKI MAONESHO YA MADINI GEITA -2022

Afisa Usalama wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Dhahabu Buckreef Charles Kafuku (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo kwa mgeni aliyetembelea Banda la Kampuni hiyo Bw. Roy Mwinga (wa pili kulia) aliyemuwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara wa Zambia katika Maonesho ya Madini yanayofanyika Mkoani Geita.
(PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO) GEITA
Mwakilishi wa Waziri wa Viwanda na Biashara wa Zambia katika Maonesho ya Madini yanayofanyika Mkoani Geita Bw. Roy Mwinga (wa tatu kulia) akitia saini katika kitabu cha wageni katika Banda la Buckreef katika maonesho hayo. 
Mjiolojia wa Kampuni ya Buckreef Francis Kiyumbi (wa pili kushoto) akionesha sampuli za aina ya miamba inayopatikana kwenye Mgodi wa Buckreef.  
Watumishi wa Mgodi wa Buckreef wakiwa katika picha ya pamoja katika Banda lao katika Maonesho ya Teknolojia katika Sekta ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili Mkoani Geita. (kutoka kushoto) ni, Afisa Usalama wa Mgodi huo Charles Kafuku, Afisa Rasirimali watu wa Buckreef, Domitilla Mang'ondi, (anayefuata), Mjiolojia Francis Kiyumbi, na Mtaalamu wa masuala ya umeme Mgodini Nahom Mramba. Muonekano wa Banda la Buckreef katika Maonesho ya Madini Mkoani Geita.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments