MwananchiHabari ZaidiKitaifa Wajumbe 663 kuamua nani awe mwenyekiti CCM Nyamagana

                           

Wajumbe 663 wamejitokeza katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Nganza jijini Mwanza kwa ajili ya kuwachagua viongozi wa CCM wilayani Nyamagana huku wagombea watatu wakiwania nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya wilaya.

Wagombea hao ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Zebedayo Athuman, aliyekuwa Mwenyekiti wa jumuiya wa wazazi wilaya ya Nyamagana, Peter Bega na Patrick Kambarage.

Awali wakipiga kampeni wagombea hao kila mmoja ameibuja na hoja yake ya kuombea kura kwa wajumbe hao ambao hawakuwa na maswali kwa wagombea wote.

Akianza kuomba kura, Zebedayo Athuman amesema akipata nafasi ya kuchaguliwa kuhudumu katika nafasi hiyo atahakikisha anaongeza mapato ya chama wilayani humo kutoka Sh20 milioni inayokusanywa kila mwezi kwa sasa.

"Nilipochaguliwa awamu iliyopita nilikuta kwa mwaka tunakusanya Sh12 milioni kwa mwezi lakini nimesimamia imeongezeka hadi hadi zaidi ya Sh20 milioni kwa mwezi, mkinichagua itaongezeka maradufu," amesema Athuman

Mgombea mwingine, Peter Bega amesema kipaumbele chake kitakuwa kuimarisha umoja ndani ya chama huku akipiga magoti kuwasihi wajumbe kumpigia kura.

"Ninazoefu wa muda mrefu ndani ya chama mkinichagua mbali na mambo mengine nitahakikisha naimarisha umoja ndani ya chama chetu," amesema Bega

Naye Patrick Kambarage ameahidi ushirikiano na kuwa daraja kati ya wanachama na uongozi wa juu ndani ya chama hicho.

"Chama chetu kinasifika kwa kudumisha ushirikiano. Ninaahidi kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanachama wa CCM tunakuwa kitu kimoja na tunashirikishana kwa kila jambo," amesema Kambarage

Baada ya kampeni hizo, wajumbe wameanza kupiga kura za kumchagua Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nyamagana Saa 6:15 asubuhi hii.

Endelea kufuatilia Mwananchi digital kwa taarifa zaidi....

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments