Mwenyekiti CCM Dodoma Abwagwa

Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Dodoma, Charles Mamba (wa kwanza kulia) ambaye amashinda, Johnick Risasi aliyekuwa Mwenyekiti na Vanessa Malesa. Picha na Habel Chidawali

 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Dodoma, Meja mstaafu Johnick Risasi ameshindwa kutetea nafasi hiyo baada ya kushindwa kwenye uchaguzi uliofanyika jana.

 Uchaguzi wa viongozi wa CCM wilaya ya Dodoma ulifanyika jana Jumamosi Oktoba Mosi, 1022 chini ya usimamizi wa Mkuu wa Wilaya Jabir Shekimweri.

Risasi ameshindwa na aliyekuwa mjumbe wa Kamati ya Siasa, Charles Mamba ambaye alipata kura 1094 kati ya kura 1344 zilizopigwa sawa na asilimia 73.1.

Akitangaza matokeo hayo jana usiku, Shekimweri alitaja idadi ya kura alizopata Meja mstaafu Risasi kuwa ni 206 wakati mgombea wa tatu Vanessa Malesa yeye alipata kura 21.

Kwa matokeo hayo, CCM Dodoma mjini itaongozwa na viongozi wapya kwa sehemu kubwa baada ya Wenyeviti wa Jumuiya za vijana, wazazi na UWT kupoteza Viti vyao vikichukuliwa na Wengine wapya licha ya Mwenyekiti wa Vijana hakugombea.

Wengine waliochaguliwa ni wajumbe wa Halmashauri Christina Kamunya, Christina Mlugu, Jesca Mbogoni na Bushura Mohamed (kundi la Wanawake).

Kundi la vijana walichaguliwa Enock Mwaliko, Fredrick Mwinje, Chris Madaha na Happy Mwajunga wakati wajumbe kundi la Wazazi ni Mussa Luhamo na Adam Msendo.

Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Taifa walichaguliwa Anthony Kanyama, Neema Mkobalo na Julian Bruno wakati mkutano wa mkoa ni Hawa Pyuza na Taus Ayubu.

Uchaguzi huo ukimalizika saa 8.20 usiku kwa kumchagua Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi, Aman Muragizi na wajumbe watatu wa kamati ya siasa.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments