Kampuni ya uchimbaji madini ya Tembo Nickel inatarajia kutoa Sh30 bilioni kama fidia kwa wananchi wilayani Ngara Mkoa wa Kagera waliopo eneo la mgodi wa uchimbaji madini ya Nickel.
Meneja mkaazi wa Kampuni ya Tembo Nickel nchini Tanzania, Benedict Busunzu ameyama hayo leo Ijumaa, Septemba 30, 2022 mbele ya Waziri wa Madini, Dk Doto Biteko alipotembelea mgodi huo uliopo wilaya ya Ngara kuona maendeleo ya uchimbaji huo.
"Eneo linalopaswa kufanyiwa uthamini ni hekta 4,100 na hekta 2,800 sawa na 70 asilimia limeshafanyiwa uthamini ambapo katika eneo hilo wamo watu wenye nyumba, mashamba, shule na maeneo ya kuabudia," amesema Busunzu bila kutaja idadi ya watu
Awali, Waziri Biteko ameitaka kampuni ya Tembo Nickel kutoa fedha za fidia kwa wananchi ambao wameshafanyiwa tathimini ya mali zao hekta 2,800 ili wananchi hao waanze kuona faida ya kuwepo kwa madini ya Nickel katika maeneo yao.
"Ili eneo la mradi likue tunategemea ushirikiano wa wananchi wa Ngara waulee huu mradi ili miaka miwili hadi mitatu ijayo maisha ya wananchi wa Ngara yaweze kubadilika," amesema Biteko
Mmoja wa wananchi wanaotarajia kupata fidia, Kerezensia Philimon amesema walishazuiwa kufanya shughuli za kilimo kwenye maeneo yanayotarajiwa kufidiwa na walipo hawana chakula waharakishiwe kupewa fidia ili wahame maeneo hayo
0 Comments