Wazee Kibaha Wataka Bima Za Afya

Katibu wa Umoja wa Wazee, Visiga Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoani Pwani, Deodatus Mbena amesema moja ya changamoto yao kubwa ni ukosefu wa bima ya afya hali in ayowafanya kushindwa kupata huduma za matibabu kwenye Hospital na Vituo mbalimbali vya afya.

Amezungumza hayo leo Jumamosi Oktoba Mosi, 2022 wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee waliyoadhimisha Mjini Kibaha amesema changamoto ya bima ya afya imekuwa ikiwafanya wazee hao kuishi kwa hofu na wasiwasi.

"Wazee hatuna uwezo wa kutafuta pesa kwa sasa na gharama za matibabu ni kubwa hivyo tunakuwa na shida pindi tunapougua tunaomba Serikali na wadau wengine watusaidie"amesema.

Mwenyekiti wa Umoja huo, Kata ya Visiga, Fatma Ally amesema kuwa mbali na changamoto hiyo pia wanahitaji eneo watakalojenga kituo salama cha matunzo na kituo cha kulea watoto yatima.

"Tunahitaji tupate eneo Ili tujenge majengo yatakayotumika kuhudumia wazee wenye matatizo mbalimbali ya kiafya pamoja na watoto yatima hivyo tunaomba Serikali na wadau wengine wajitokeze Ili kutuunga mkono"amesema

Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibaha, Sozi Ngate amesema kuwa kwa sasa Halmashauri za Mji na Wilaya ya Kibaha zinaendelea na utaratibu wa kuwatengenezea vitambulisho wazee vitakavyowawezesha kupata matibabu kwenye Hospital na Vituo vya afya ndani ya mkoa huo.

Amesema kuwa Serikali ipo pamoja na wazee kwani inatambua mchango wao katika masuala ya kijamii na kiuchumi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments