BINGWA MTETEZI ATOA DOZI NENE KOMBE LA DUNIA

 Mabingwa watetezi wa Michuano ya Kombe la Dunia, Ufaransa wamepata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya timu ya taifa ya Australia, katika dimba la Al Janoub kwenye mchezo wa Kundi D la Michuano hiyo inayoendelea nchini Qatar.Licha ya kuandamwa na majeruhi wengi katika Kikosi chao, Ufaransa walipata ushindi huo kupitia mabao ya Kiungo Mkabaji Andrien Rabiot dakika ya 27’,  mabao mengine yamefungwa na Mshambuliaji Olivier Giroud dakika 32’ na 71’ na Kylian Mbappé dakika ya 68’, huku bao la Australia limefungwa na Craig Goodwin dakika ya 9’.

Katika mchezo huo, Mshambuliaji wa Ufaransa, Olivier Giroud amefunga mabao mawili na kuwa Mfungaji bora wa muda wote katika timu hiyo ya taifa akifikia rekodi ya Mshambuliaji wa zamani Thierry Henry mwenye mabao kama hayo akicheza michezo 123.

Ufaransa wanaongoza Kundi D la Michuano hiyo, wakiwa na alam Tatu huku nafasi ya pili akiwa Tunisia mwenye alama moja sawa na Denmark wenye alama kama hizo, huku Australia wakiburuza mkia bila alama yoyote.

Post a Comment

0 Comments