CAMEROON HALI SI SHWARI KOMBE LA DUNIA.

 Licha ya kucheza soka safi na kulazimishana sare ya mabao 3-3 dhidi timu ya taifa ya Serbia, timu ya taifa ya Cameroon ipo kwenye sehemu si salama kwao kutokana na kuwa na alama moja pekee katika michezo miwili ya Kundi G ya Michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar.

Katika mchezo huo dhidi ya Serbia uliopigwa kwenye dimba la Al Janoub, Cameroon walionyesha soka safi na kufanikiwa kupata sare hiyo baada ya kutanguliwa mabao 3-1. Mshambuliaji Vincent Aboubakari aliyeingia kipindi cha pili alirudisha uhai kwa Simba Wasioshindika katika mchezo huo.

Kwenye mchezo huo, mabao ya Cameroon yalifungwa na Jean-Charles Castelletto dakika ya 29', Vincent Aboubakar dakika ya 63' na bao la tatu likifungwa na Jean Eric Choupo-Moting 66'. Mabao ya Serbia yalifungwa na Strahinja Pavlović dakika ya 45+1', Sergej Milinković-Savić dakika ya 45+3’ na Aleksandar Mitrović dakika ya 53'

Msimamo wa Kundi hilo, Brazil anaongoza akiwa na alama tatu, sawa na Switzerland wenye alama kama hizo, huku Cameroon na Serbia wakiwa kwenye nafasi ya tatu na nne wakiwa na alama moja pekee.

Kikosi cha Rigobert Song kitakuwa na kibarua kizito katika mchezo wa mzunguko wa tatu dhidi ya timu ya taifa ya Brazil huku Serbia wakiwa na kibarua dhidi ya Switzerland, michezo hiyo itaamua timu mbili zitakazofuzu hatua ya 16 Bora ya Michuano hiyo.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments