CCM YASEMA SHAHADA YA HESHIMA YA UDAKTARI WA FALSAFA NI UTHIBITISHO WA KAZI KUBWA ANAZOZIFANYA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

Chama Cha Mapinduzi (CCM) tumeguswa na kufurahishwa na uamuzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kumtunuku shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mahafali ya 52 duru ya 5 yaliyofanyika leo Jumatano 30 Novemba, 2022 ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Uamuzi huo ni uthibitisho wa dhahiri wa kazi kubwa na nzuri zinazofanywa na serikali ya CCM, awamu ya sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuleta ustawi wa maisha na maendeleo endelevu kwa Nchi yetu. 

Kati ya kazi kubwa zlizofanyika na kutumika kumtunuku shahada hiyo ya heshima ni pamoja na mageuzi ya kiuchumi, uimarishaji wa misingi ya demokrasia, utawala bora, maendeleo ya jamii, ameleta furaha na tumaini jipya miongoni mwa wananchi ambayo yote ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 uliochagizwa na utashi wake wa kisiasa, ukomavu na umahiri alionao katika uongozi wake.

Shahada hii ya heshima ni fahari kwa  Chama Cha Mapinduzi  na watanzania wote kuwa tunaye Rais anayewajibika kwa maslahi ya wote na tunaimani ya kwamba 
itampa moyo kuwa watanzania wanaona kazi nzuri anazozifanya kwa Taifa hivyo kumpa ari na nguvu ya kuendelea kutekeleza wajibu wake.

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
Itikadi na Uenezi.
30 Novemba, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa wa Heshima ikiwa ni Shahada ya Udaktari wa Juu katika Humanitia na Sayansi Jamii na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa Cheti mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa wa Heshima ikiwa ni Shahada ya Udaktari wa Juu katika Humanitia na Sayansi Jamii na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolph Mkenda, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa William Anangisye kwenye picha ya pamoja na viongozi wengine wakati wa Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika tarehe 30, Novemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Wahitimu mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments