DKT. MWIGULU MGENI RASMI MAHAFALI CHUO CHA KODI

Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Prof.Isaya Jairo akizungumza na Waandishi wa habari leo Novemba 23,2022 Jijini Dar es Salaam kuelekea katika Mahafali ya 15 ya Chuo hicho  yatakayofanyika Novemba 25 mwaka huu.

 

WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt.Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 15 ya Chuo cha Kodi (ITA) ambayo yatafanyika Novemba 25,2022 chuoni hapo Jijini Dar es Salaam.

 
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Novemba 23,2022 Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Prof.Isaya Jairo amesema jumla ya wahitimu 489 wanatarajiwa kutunukiwa vyeti, Stashahada, Shahada na Stashahada ya Uzamili katika kozi mbalimbali zinazotolewa na Chuo hicho.
 
Amesema ukilinganisha na wahitimu 387 wa mwaka jana 2021, hili ni ongezeko la asilimia 25.1 ya wahitimu wa mwaka huu 2022.
 
“Ongezeko hili linatokana na jitihada za Chuo kuhakikisha viwango vya mafunzo yanayotolewa na Chuo vinakidhi matakwa ya mahitaji ya taaluma na kodi”. Amesema Prof. Jairo.
 
Aidha amesema kwa kuzingatia mahusiano na ushirikiano uliopo kati ya Chuo na Mamlaka za Mapato za Afrika, Chuo kimewaalika baadhi ya Wakuu wa Mamlaka za Mapato mbalimbali ambapo tayari baadhi wamethibitisha kushiriki wakiwemo Mamlaka za Mapato Ghana, Kenya, Eswatini na Malawi.
 
Amesema pamoja na Chuo kutoa mafunzo, pia kinatoa ushauri na kuwajengea uwezo watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) na Mamlaka zingine za Mapato Afrika.
 Chanzo ,Michuzi 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments