GRACE SAMWELI AIBUKA MSHINDI UENYEKITI UWT MKOA WA SHINYANGA, MAGRETH COSMAS ASHINDWA KUTOBOA

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuia ya Umoja wa wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) mkoa wa Shinyanga wamemchagua Grace Samweli kuwa mwenyekiti wa Umoja huo baada ya kumshinda Magreth Cosmas aliyekuwa anatetea nafasi hiyo kwa kupata kura 180 dhidi ya wapinzani wake Magreth Cosmas aliyepata kura 130 na Angela Paul kura 10.

Akitangaza matokeo hayo leo Alhamis Novemba 17,2022 Msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo Sauda Salum Mtondoo ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Igunga amesema kuwa wajumbe halali wa mkutano huo walikuwa 321 kura halali 320 na kura moja imeharibika.


Aidha amewashukuru wajumbe kwa ushirikiano na demokrasia walioyoionesha katika uchaguzi huo ambao umefanyika kwa uhuru na amani.


Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika nafasi hiyo Grace Samwel amewasii wajumbe kuwa wamoja na kuvunja makundi waliyotengeneza wakati wa mchakato wa uchaguzi ili kuendelea kukijenga chama hicho.


“Nimpongeze aliyekuwa mwenyekiti wa UWT wa mkoa huu Magreth kwa uongozi wake wa miaka mitano iliyopita nitashirikiana nae katika uongozi wake sambamba na kuendeleza yale aliyoanzisha,”amesema Samweli.

Kwa upande wake aliyekuwa mwenyekiti wa UWT mkoa wa Shinyanga Magreth Cosmas amempongeza Grace Samweli kwa ushindi alioupata na kuwaomba wajumbe kumuunga mkono mwenyekiti aliyechaguliwa katika utekelezaji wa majukumu yake mapya ya kuiongoza jumuia hiyo.


Nao baadhi ya wajumbe walioshiriki katika uchaguzi huo akiwemo mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Santiel Kirumba pamoja na Lucy Mayenga wameeleza kuwa baada ya uchaguzi kumalizika wataendelea kukipigania na kukijenga chama hali itakayosaidia kuchochea maendeleo ya chama hicho.
Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments