IRAN WAAMKA KOMBE LA DUNIA

Timu ya taifa ya Iran imeamka katika Michuano ya Kombe la Dunia baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wales katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Kundi B uliopigwa kwenye dimba la Ahmad Bin Ali nchini Qatar.


Katika mchezo huo uliokuwa wa kasi muda wote mabao ya Iran yamefungwa na Rouzbeh Cheshmi dakika ya 90+8' na Ramin Rezaeian kwenye dakika ya 90+11'. Mabao yote yamefungwa na Wachezaji wenye asili ya Ulinzi wakiwa uwanjani.

Iran walipoteza mchezo wao wa mzunguko wa kwanza wa Michuano hiyo baada ya kufungwa mabao 6-2 dhidi ya timu ya taifa Uingereza, huku Wales wakipata sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya taifa ya Marekani.

Msimamo wa Kundi hilo, Uingereza anaongoza akiwa na alama sita akiwa na mchezo mmoja pekee, huku Irani nafasi ya pili wenye alama tatu wakiwa na michezo miwili, Marekani nafasi ya tatu na alama moja sawa na Wales. Uingereza anakutana na Marekani katika mchezo wa mzunguko wa pili.
 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments