KAMPENI YA KUPINGA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA YA BARRICK YAWAFIKIA WAKAZI WA DAR

Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za wilaya ya Kinondoni wakishiriki katika maandamano hayo ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.
****
Kampuni ya Barrick imeungana na wadau mbalimbali kuadhimisha Siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ambapo imeshiriki kuendesha kampeni dhidi ya vitendo hivyo katika maeneo yanayozunguka migodi yake ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi.

Jijini Dar es Salaam kampuni kwa kushirikiana na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi imeandaa maandamano yaliyohusisha wananchi mbalimbali wakiwemo wanafunzi kutoka shule mbalimbali za wilaya ya Kinondoni yaliyofanyika katika viwanja vya kituo cha Polisi cha Oysterbay.

Kupitia hafla hiyo jumbe mbalimbali kuhusiana na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zilisomwa baada ya maandamano hayo. Kauli mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho hayo ni "Tokomeza Mauaji na ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto".

Meneja wa Barrick nchini Georgia Mutagahywa akiongea baada ya maandamano ya Kupinga vitendo vya ukatili wa Kijinsia.
Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Aloyce Nyantora akiongea wakati wa hafla hiyo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Stela Msofe akiongea wakati wa hafla hiyo
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za wilaya ya Kinondoni wakishiriki katika maandamano hayo ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Washiriki wa maandamano wakipiga picha ya pamoja kwenye hafla hiyo.
Washiriki wa maandamano wakipiga picha ya pamoja kwenye hafla hiyo.
Washiriki wa maandamano wakipiga picha ya pamoja kwenye hafla hiyo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments