Kawaida Mwenyekiti Mpya UVCCM Taifa

Wajumbe wa mkutano mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wamemchagua Mohamed Ali Mohammed (Kawaida) kuwa mwenyekiti mpya wa umoja huo.

Kawaida ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Kusini Unguja anachukua nafasi ya Kheri James ambaye Juni 2021 Rais Samia Suluhu Hassan alimteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo.

Kawaida amepata kura 523 akiwashinda Farid Mohammed Haji aliyepata kura 25, Kassim Haji Kassu kura 2 na Abdallah Ibrahim Natepe aliyepata kura 1.


Akitangaza matokeo hayo Jana  Jumapili Novemba 27,2022 Jijini Dodoma msimamizi mkuu wa uchaguzi huo ambaye ni Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alimtangaza Kawaida kuibuka na ushindi huo.

Mara baada ya kumtangaza wajumbe walianza kuimba Kawaida Kawaida huku wakimbeba kuelekea mbele ya ukumbi.TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments