Kinana Aahaidi Ushirikiano na Cuba Kuendelea

Wakati ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba ukitimiza miaka 60 tangu kuanzishwa kwake, Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana amezunguzia mambo mbalimbali ya kukumbukwa.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana ameahidi kuendelea ushirikiano uliodumu kwa miaka 60 sasa katika nyanja mbalimbali baina ya vyama, Tanzania na Watanzania na nchi ya Cuba.

Ahadi hiyo inakuja miaka sita baada ya Rais wa Cuba, Fidel Casto kufariki dunia na madhimisho ya miaka 100 tangu Rais wa kwanza wa Tanzania, Julius Nyerere kuzaliwa.

Kinana ameyasema hayo leo Novemba 25, 2025 wakati akizungumzia kuhusu ushirikiano ya Cuba na Tanzania kutimiza miaka 60 tangu uanishwe.

Amesema Tanzania imekuwa na ushirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwemo za elimu, afya na Kilimo kwa miongo sita, ushirikiano ambao umeirishwa na misimamo yao inayolingana katika masuala ya msingi.

“Tanzania na Cuba imekuwa na mchango wa hali, mali na maisha katika ukombozi wa Bara la Afrika. Uhusiano wa karibu kati ya Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere na Fidel Casto. Nchi hizi zimesaidia kuharakisha ukombozi wa bara la Afrika,”amesema.

Amesema viongozi hao watakumbukwa kwea ushirikiano wao wa karibu katika mambo mbalimbali ya msingi kama vile kupambana na dhuluma na utetezi wa haki za binadamu na kupambana na unyanyasaji na uonevu dhidi ya mataifa madogo.

Amesema hata baada ya hapo Cuba imeendelea na ushirikiano katika sekta za kiuchumi miongoni mwa nchi za kusini mwa dunia.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments