KMC FC KUWAFUATA SINGIDA BIG STAR KESHO NA NYOTA 20.

 Kikosi cha KMC kesho kitaanza safari kuelekea mkoani Singida kwa ajili ya mchezo mwingine dhidi ya Singida Big Star utakaochezwa Novemba 23 saa 14:00 mchana katika Uwanja wa Liti mkoani humo.


Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni , itaondoka na wachezaji 20 na kwamba kabla ya kuanza safari mapema asubuhi ya leo imefanya mazoezi ya mwisho kama sehemu ya kuendelea kujiweka sawa katika mchezo huo.

KMC FC itakuwa ugenini  ikiwa imetoka kupoteza mchezo dhidi ya Dodoma Jiji uliopigwa Novemba 15 katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es na kwamba inakwenda Singida ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo muhimu ikiwa nyumbani.

Katika mchezo huo , Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu Thierry Hitimana imejipanga kuhakikisha kwamba inafanya vizuri licha ya kuwa Singida Big Star ni Timu nzuri ambayo pia inahitaji matokeo kutokana na kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Yanga katika uwanja wa Benjamini Mkapa.

"Tunakwenda kupambana kwa mara nyingine ugenini, mchezo utakuwa mgumu kutokana na wapinzani ambao tunakwenda kukutana nao pia wametoka kupoteza kama ilivyo kwetu, ila pamoja na ushindani huo KMC FC tunawachezaji bora wenye uwezo mkubwa wakuipambania Timu kupata matokeo mazuri.

"Hakuna mchezo mwepesi , tunahitaji zaidi ushindi , wachezaji wote wapo imara na kila mmoja yupo tayari kuipambania Manispaa yetu ya Kinondoni , hatukuwa na wakati mzuri kwenye michezo miwili ambayo tulikuwa Kanda ya Ziwa, hivyo mashabiki zetu msiwe na hofu kwasababu sikuzote  Timu bora huwa haipoteza  mechi mara mbili.

Kwa upande wa Afya za wachezaji, Matheo Anton ambaye hakuonekana kwenye michezo miwili tayari amerejea kikosini na wenzake, Awesu Ally Awesu ameanza mazoezi mepesi  ya peke yake, lakini pia tunaongezeko la wachezaji wawili wenye majereha ambao ni Emmanuel Mvuyekure pamoja na Kelvn Kijiri  na kwasasa wanaendelea na matibabu.TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments