MCHENGERWA ASHINDA NAFASI YA MNEC MKOANI PWANI, ASEMA ANA DENI LA KULIPA

 Nyota wa Kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo rasmi ameondoka katika Klabu ya Manchester  United baada ya makubaliano ya pande zote mbili kati ya Mchezaji huyo na timu hiyo.

“Kutokana na kutoelewana kati ya mimi na Klabu, nimeamua kufika makubaliano na Klabu kuondoka mapema iwezekanavyo”, Kauli ya Ronaldo.Ronaldo ameondoka Man United, baada ya  mahojiano yenye utata ambapo aliikosoa Klabu hiyo, huku akinukuliwa kuwa hakumuheshimu Kocha Mkuu wa timu hiyo, Erik ten Hag.

“Klabu inamshukuru Ronaldo kwa mchango wake ndani ya timu muda wote akiwa hapa Old Trafford”, imeeleza taarifa iliyotolewa na Manchester United.

“Tunamtakia kila la kheri yeye na Familia yake huku mbele, sisi katika timu yetu tunaendelea kupambana na Kocha Erik ten Hag tukifanya kazi pamoja ili kufika mafanikio ndani ya timu.”

Imeelezwa, Cristiano Ronaldo amebakisha miezi saba kwenye mkataba wake wa  £500,000 kwa wiki ndani ya Manchester United sasa anaondoka Klabuni hapo na anaweza kusaini timu nyingine dirisha la usajili mwezi Januari.

Kwa sasa, Ronaldo yupo nchini Qatar kwenye Michuano ya Kombe la Dunia na timu ya taifa ya Ureno ambapo wataanza kucheza mchezo wao wa kwanza siku ya Alhamisi dhidi ya timu ya taifa ya Ghana.

Nyota Cristiano Ronaldo alisajiliwa Manchester United, Agosti 2021 akitokea Klabu ya Juventus ya Italia.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments