MKUU WA WILAYA YA UBUNGO AFUNGUA KIKAO KAZI CHA WATAALAM WA BAJETI WA HALMASHAURI NA MADIWANI KILICHORATIBIWA NA TGNP

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James amefungua mkutano wa Wataalam wa Bajeti za Halmashauri ambao ni Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na Madiwani kilichoratibiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) leo tarehe 21 hadi Novemba 24 mwaka 2022 ili kuwajengea uwezo kwenye suala la utengaji wa Bajeti kwa mlengwa wa usawa wa Kijinsia.


Akizungumza wakati wa kufungua Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James amesema ni faraja kubwa kuona kuwa mafunzo haya ya “Uandaaji wa Bajeti kwa Mrengo wa Kijinsia yameleta pamoja maafisa mipango na bajeti, maendeleo ya jamii na waratibu wa madawati ya jinsia kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, wawakilishi kutoka ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Halmshauri za wilaya ya Kishapu, Mbeya, Kasulu, Morogoro, Tarime, Same, Muheza na Moshi. Na nimeambiwa pia, Kwa Dar es salaam kuna washiriki kutoka manispaa za ubungo, Kinondoni, Ilala na Temeke.

Pia amesema mafunzo hayo watapata fursa ya kujifunza na kujadiliana namna ya kuchambua vipaumbele vya jamii kwa mrengo wa kijinsia kama sehemu muhimu ya maandalizi ya bajeti na mipango mingine ya seriakali/Taifa.

"Naomba tuyazingatie haya na tuweze kuyafanyia kazi ili mwisho wa siku, matunda ya mafunzo haya yanapatikana. Bajeti yenye mrengo wa kijinsia ni jambo la msingi sana kwa maendeleo na ustawi wa mtu mmoja mmoja, jamii na Taifa kwa ujumla." Alisema Jemes

Amesema ni jukumu letu kama Halmashauri kwa kushirikiana na asasi za kiraia hususani Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kuhakikisha mchango wa kila mmoja wetu katika eneo hili unaonekana ili kuwa na maendeleo endelevu kwa makundi yote ni lazima bajeti zetu ziweze kuonesha mgawano sahihi wa rasilimali kulinga na kila kundi.

"Juhudi za Serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imetekeleza kwa vitendo kuhakikisha masuala ya kijinsia yanapewa kipaumbele na kutekelezwa." alisema Kheli James

Mkuu wa Wilaya ametoa shukrani za dhati kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi, Bodi ya Wakurugenzi, wanachama na wafanyakazi kwa kunipa heshima hii kubwa ya kuwa Mgeni Rasmi katika kufungua mafunzo haya muhimu sana katika mustakabali wa taifa letu. Napenda pia, kutambua na kutoa pongezi zangu za dhati kwa shirika la TGNP kwa kuratibu mafunzo haya.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi amesema malengo ya mafunzo haya ni kutoa fursa kwa washiriki kujadiliana, kushirikishana uzoefu, kujenga maarifa na ujuzi na kuweka mikakati ya pamoja ya kuhakikisha bajeti zetu zinakuwa za mrengo wa kijinsia na kujenga uelewa wa pamoja wa ujumuishaji wa masuala ya kijinsia kwenye mipango na bajeti na namna ya kuandaa bajeti yenye mrengo wa kijinsia, fursa zilizopo na changamoto tunazokutana nazo wakati wa kutenga bajeti kwa mrengo wa kijinsia kama zipo.

Pia Liundi ameiomba Serikali kuongeza kazi zenye staha, fursa za ufikiwaji, umiliki, upatikanaji na udhibiti wa rasilimali za uzalishaji kwa wanawake na kuendeleza uchumi unaozingatia usawa wa kijinsia ili kuleta maendeleo endelevu katika nchi

"Nina matumaini kwamba baada ya mafunzo haya tutarudi tena kupeana mrejesho wa utekelezaji wake na nawaomba tukachape kazi kazi iendelee kwa vitendo katika Halmashauri zetu, tupate maisha bora kwa kila mwananchi" Alisema Liundi
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James akizungumza na Wataalam wa Bajeti za Halmashauri ambao ni Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na Madiwani kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini wakati wa kufungua mafunzo yanayofanyika kuanzia leo tarehe 21 hadi 24 Novemba, 2022 yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo Wataalam wa Bajeti za Halmashauri ambao ni Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na Madiwani kutoka Halmashauri mbalimbali wakati wa  ufunguzi wa mafunzo yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Jinsia kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Linus Kahendaguza akizungumza kuhusu namna wanavyotekeleza mipango mbalimbali yenye mlengo wa usawa wa kijinsia pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James kwa ajili ya kufungua  warsha kwa Wataalam wa Bajeti za Halmashauri kutoka katika Harmashauri mbalimbali iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wataalam wa Bajeti za Halmashauri ambao ni Maafisa Mipango na Bajeti, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Madiwani kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini pamoja na  wafanyakazi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wakifuatilia hituba ya mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James ilipokuwa anafungua warsha kwa wataalam hao yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika jijini Dar es Salaam. 
Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James akiwa kwenye picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wakati wa kufungua warsha kwa Wataalam wa Bajeti za Halmashauri kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James akiwa kwenye picha za pamoja na Wataalam wa Bajeti za Halmashauri ambao ni Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na Madiwani mara baada ya kufungua warsha hiyo iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Same Yusto Mapande akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James kwa kuweza kufungua warsha kwa Wataalam wa Bajeti za Halmashauri yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika katika Hoteli ya Sea Shells kuanzia leo tarehe 21 hadi 24 Novemba, 2022.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments