NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA NDUGU MNDEME AFUNGUA SEMINA YA SIKU 1 YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI DODOMA

 

 Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndugu Christina Mndeme akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya fidia kwa wafanyakazi na wadau iliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) iliyofanyika leo Novemba 30, 2022 katika ukumbi wa White House jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndugu Christina Mndeme akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mduma wakati wa ufunguzi wa semina ya fidia kwa wafanyakazi leo Novemba 30, 2022 katika ukumbi wa White House jijini Dodoma.

Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga (kulia) akichangia mada wakati wa semina ya fidia kwa wafanyakazi iliyofanyika kwenye ukumbi wa White House jijini Dodoma. 
 

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndugu Christina Mndeme ametoa wito kwa wafanyakazi nchini ya kujikinga na majanga wanapokuwepo kwenye maeneo ya kazi.

Naibu Katibu Mkuu ameyasema hayo leo jijini Dododma wakati wa ufunguzi wa semina ya siku 1 ya Fidia kwa Wafanyakazi iliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)
“Naomba kuchukua fursa hii kuziagiza taasisi zote kulipa michango ya nyuma wanayodaiwa sasa” Alisema Ndugu Mndeme.

Kwa upande Mwingine Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Dkt. John Mduma amesema mchango mkubwa wa mfuko huo ni kuhakikisha Watanzania hawapati madhara na kuingia kwenye wimbi la umasikini pale wanapopata matatizo sehemu za kazi ikizingatiwa kuwa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 ibara ya 30 kifungu kidogo D imetaja kinaga ubaga masuala ya fidia kwa wafanyakazi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments