RAIS SAMIA AIPONGEZA CCM MANYARA KWA UCHAGUZI USIO NA PURUKUSHANI

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwasili katika jengo jipya la ofisi ya Mkoa wa Manyara lililopo mjini Babati kwa ajili ya kulizindua, akiwa katika ziara y siku mbili mkoani Manyara. (Picha zote na Fahad Siraj wa CCM).


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kamati ya Siasa ya CCM katika ofisi za Chama Mkoa wa Manyara mjini Babati, akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani Manyara.

*Pia asifu ujenzi wa jengo la Chama la kisasa

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Samia Suluhu Hassan amewapongeza wana CCM Mkoa wa Manyara kwa kukamilisha uchaguzi wa Chama ngazi ya mkoa bila ya purukushani.

Pia, amewapongeza wana CCM kwa kujenga jengo la kisasa la ofisi ya Chama la Mkoa huo na kusema wameonyesha ukomavu na kukipenda Chama chao.

Rais Samia ameyasema hayo leo Babati mkoani Manyara akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya siku mbili mkoani humo akiambata na viongozi mbalimbali akiwemo mlezi wa CCM katika Mkoa huo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka.

"Niwapongeze kwa kumaliza uchaguzi salama. Mmemaliza uchaguzi salama, mmeshachagua wenyeviti wenu wa mkoa wa Chama, wa wilaya na jumuiya kwa salama. Na kwa Manyara hatukusikia purukushani kwa kwa hiyo hongereni sana. Hii inaonyesha ukomavu katika Chama, tunawapongeza sana” alisema na kuongeza

"Nakupongezeni wana CCM kwa michango yenu na kufikisha hatua hii ya jengo, hii inaonyesha kabisa kwamba wanachama wameshiba Chama chao na wanataka kuona maendeleo ya Chama chao. Kwa hiyo hongereni sana.

Tumeona hatua za ujenzi, pamoja nami kuna Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, ndugu yetu Shaka (Shaka Hamdu Shaka) lakini nami Mwenyekiti tumeona maendeleo yenu tumesikia changamoto, tumeona mlipofika kwa hiyo tunaomba tuachieni kidogo nasi tukajipange kuona tunaweza kusaidia kiasi gani lakini kwa ujumla nikupeni hongera sana," amesema.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments